Mwanafunzi ambaye anataka kupata alama
za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia
dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya
kuishi kwa kutegemea bahati.
KWANZA: Kama nilivyosema hapo juu jambo
la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na
kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika
alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa
kwake.
PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku
ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia
shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye
mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya
nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha
hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu
si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao
huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha
maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake
na hivyo kujiandaa.
Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile
nilichosema awali, yaani kuwa na
kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia
ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia
rudia.
TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo
huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri
kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako
hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.
NNE: Hakikisha unajizoeza kufanya
mitihani ya majaribio mara kwa mara,
ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya
kufanya mtihani halisi. Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa
darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama
amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.
TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri
unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo
ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi
hata kila siku.
SITA: Angalia kwa makini alama zako za
mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji
nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au
yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
SABA: Ili mwanafunzi awe na uhakika wa
kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye
kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema
kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu, baadhi ya wanafunzi hukesha
wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa
kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
TISA: Kabla mwanafunzi hajaingia katika
chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu. Eneo hili ni muhimu
sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na
hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani. Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa
kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya
mtihani bila hofu.
KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio
ya mwanafunzi, haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi.
Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA
NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini
mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.
umesahau la kwanza kabisa ni kumshirikisha mungu
ReplyDeleteHakika kabisa, Mungu kwanza mengine baadaye.
DeleteMungu kwanza
ReplyDeletehasante kwa kuandaa makala hii pia naombaa kuongezea jambo lingine ulilo sahau kuliandika ,ili mwanafunzi awe na kumbukumbu inatakiwa ale ndizi mbivu, nanasi,tikiti,na vyakula vyote vyenye omega-3-S-fatty acid hii omega-3S-fatty acid ambayo husababisha mwanafunzi au binadamu yeyote kuto kusahau. hiyo omega 3 s fatty acid inapatikana kwenye samaki, mbegu za mlonge (moringan seeds),mbegu za maboga nk. kwa ushauri nitafute BURE BILA MALIPO 0787433103 au 0713202420 Pia ushauri jinsi ya kusoma natoa bure kwa wanafunzi wote na wana vyuo vikuu
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletekweli ni njia nzurti ukizifuata utafanikiwa
ReplyDeleteHoja nzuri Sana,ikiwa zitazingatiwa bila Shaka patakuwepo matokeo ya kuridhisha.shukrani Kwa mwelekezi pamoja na wachangizi
ReplyDeleteTNKS FOR THE ADVICE
ReplyDeleteThnx 4Ur Advice let me try working on it.
ReplyDeleteThx 4ur advice God bless U let me try working on it
ReplyDeleteNi Jambo la Faraja Ssna
ReplyDelete