Fursa na mawazo mbalimbali ya biashara yanatoka
katika mazingira yanayotuzunguka; majumbani, makazini, mashuleni, safarini
n.k Wajasiriamali waliofanikiwa hupata
mawazo ya kuanzisha biashara, kuwa makini na kulifanyia kazi wazo la biashara
alilolivumbua katika mazingira yanayomzunguka.
Ni vema ukatoka nje kujichanganya na watu ili uone
fursa mbalimbali zilizopo kwa muda huo ambazo zitaweza kukusaidia ukatoa
maamuzi ya kuanzisha biashara yako huku ukikutana na wafanyabiashara
waliotangulia kwa kuiga tabia za kisiriamali. Kuna usemi usemao “mvumbuzi sio
tu kufumbua kitu bali ni uchakarikaji wa kutafuta fursa na mawazo sahihi ya
kuanzishisha biashara”.
Njia 3 za kuvumbua wazo sahihi la biashara
Kwa kujifunza kupitia kwa wengine wanaotuzunguka,
utakutana na mawazo mbalimbali na ndio njia ya kupata majibu ya kukuwezesha
kujua ni biashara gani uanzishe. Kuna njia tatu za kufuata:-
1. Weka orodha ya mawazo yako
Hakuna biashara isiyolipa; utashangaa mtu mmoja
anafungua biashara leo inakufa baada ya miezi sita. Lakini jirani yake ndani ya
miezi sita anafungua na biashara nyingine ama kupanua maradufu biashara yake.
Kila siku ongeza angalau fursa moja kwenye daftari lako. Usichague fursa; zote
ni nzuri kama ukiwa na mipango na malengo.
Usikate tama, jiulize kwa nini hawa wameweza na kwa
nini wewe ushindwe? Jipe moyo “hashindwi mtu hapa” Uhondo wa ngoma uingie
ucheze mwenyewe. Na mara nyingine matatizo ndio hupelekea mtu kujikuta
anaangukia kupata wazo sahihi la biashara.
2. Toka nje, jichanganye na watu
Mawazo ya kibiashara hayapatikani kwa kukaa ndani na
kusubiri wazo lishuke kutoka mbinguni. Unahitajika ubunifu ambao unaweza
kuupata kupitia maonyesho ya biashara, kutembelea wafanyabiashara wazoefu na
kubadilishana mawazo. Ikiwezekana “wawinde” wafanyabiashara unaowafahamu ambao
unaweza kuongea kuhusu wazo lako. Ishi kwa kuangalia wanavyoendesha biashara
zao. Wengi hukatisha watu tama, usiwajali.
3. Iga
mbinu za kupambana na changamoto
Matatizo yapo kila siku, kila sehemu, muda wowote.
Biashara zote zina changamoto, jifunze ni jinsi gani wafanyabiashara
wanavyopambana na changamoto zinazowazunguka na utapata njia muafaka ya
kupambana na hivyo kuendelea na maisha. Iga na uweze kuzitumia mbinu hizo ila
kuwa makini kiga mazuri huku ukiyaacha yale mabaya.
safi sana vijana tumieni mawazo haya
ReplyDelete