Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko
sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu
alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa
Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu
atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira
ya baridi.
Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa
mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua
ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol
Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba
maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.
Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za
Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia
baina ya tarehe 17 na 24 Disemba.
Wakristo wa kale
Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani,
Wakristo wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa
vile idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua
shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea mwezi wa
Disemba kwa kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus, ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125
hadi 136 AD, askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe
wakati huu ili kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”. Hata hivyo,
kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa
Kristo, kawaida ya Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa
Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa,
kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.
Katika mwaka 274 AD, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Disemba.
Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis
Invicti”, ‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika mwaka 320 AD, Papa
Julius I aliitangaza tarehe 25 Disemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu
Kristo.
Mnamo mwaka 325 AD, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla
haikutiliwa maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa
dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe
isiohamishika kwa tarehe 25 Disemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku
kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe yenye
kuhamishika. Mnamo mwaka 354 AD, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa
wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Disemba.
Hata hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25 Disemba
kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitambua kama ni tarehe ya
sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku
hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi
ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi
cha hivi karibuni. Huko Uingereza England,
Oliver Cromwell alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka 1649 na
1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu.
Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale
Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi)
walipokimbia uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani. Hata
hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800. Na, weka
akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo.
Krismasi inaanza kuwa
maarufu
Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na
kitabu cha Washington Irving The Keeping
of Christmas at Bracebridge Hall ‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La
Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria,
alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za
mti wa Krismasi Christmas tree na
Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols
ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja
kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za Kumsifu Yesu za
Krismasi Christmas Carols (ambapo
aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza
Kuu la Marekani US Congress lilikutana Siku ya Krismasi).
Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali
kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa
ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali.
Mnamo mwaka 1860, mfananishi illustrator
wa Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu
Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi Father Christmas. Mwaka 1907, Oklahoma
ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama
ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua
Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.
Nakuombea Krismasi
Njema
Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya
Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa
inasherehekewa Disemba ya 25, wakati wa solstice.
Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Disemba 25
hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani
wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangano
wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans
– au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative
– watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa,”
wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku za hivi
karibuni.
Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi?
Mazoea ya Krismasi
Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye
kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka
yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa
ya Baba Krismasi Santa.
Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu
aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?
Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli
utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi.
Je, Krismasi Ina
Ushahidi wa Biblia?
Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya
sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa
mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):
“Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na
mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu,
wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia
10-3,4).
Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba
miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi
imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani,
Uingereza na baadaye Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa
dini miongoni mwa watu wa Tyutoniki Teutonic
na Skandinavia Scandinavia wa Ulaya
ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa ki-Jerumani walileta
mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17.
Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998)
Je, Yesu Alizaliwa
Disemba ya 25?
Si tarehe ya Disemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa
ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka
530 C.E kwamba mtawa monk aitwaye
Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni
Disemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya
kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni
Disemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia
Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja
na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani.
Mapagani wa Kirumi walisherehekea Disemba 25 kama ni ya kuzaliwa
kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.
“Mnamo karne ya pili A.D, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya
kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano
iliyo mingi” (The Concise Columbia
Encyclopedia, toleo la mwaka 1995).
‘Waungu’ wengine wakipagani waliozaliwa Disemba ya 25 ni: Hercules mtoto
wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa
Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani
0 comments: