Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika
kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na
jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na
uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa
kitaasisi na kifedha
1. Mradi
huo unaitwaje?, Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni
kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na
kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
2. Maswali
mengine ni kama ifuatavyo; Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni
ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo
lilianza nkwa nani?
3. Kwanini
tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki?, Je, mradi ni suluhisho halisi
na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu
utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
4. Unaweza
kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje katika jamii
hii.
5. Utasimamiwa
na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili kuwafikia
jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia utawalenga watu
kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?
6. Malengo
au Lengo kuu la mradi ninini? Madhumuni yake mengine ni yapi? Shughuli za mradi
na majukumu madogomadogo ninini? Ambayo lazima yapangwe kimantiki na kwa
matarajio yenye kufikia lengo.
7. Ni
wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu, mchango wa wadau
hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu ?
8. Kuna
uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala la mazingira
linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na magonjwa yasiyotibika
yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa mradi huu?
9. Umepanga
kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi huu? Uendelevu
wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu kwa namna gani?
10. Swali
linguine ni kama kuna mradi kama huu uliowahi kutekelezwa hapo au jirani na
hapo katika kipindi kifupi kilichopita.
NB: Maswali haya yakijibiwa vizuri kwa mtiririko
sahihi huitwa andiko la mradi na ifuatayo ndio mpangilio wa jumla ambao
wahisani wengi wameupenda katika kuandika andiko la mradi.
nakubaliana kabisa na hayo maswali
ReplyDelete