Leo nawaletea tabia zitakazo kufanya usipate
mafanikio kama usipobadilika na kufanya vitu venye kuleta tija katika maisha
yako. Epuka kufanya yafuatayo ili uweze kufanikiwa katika mwaka 2014
Imani
Potofu
Ni mawazo yasiyo sahihi juu ya kitu Fulani au juu ya
wewe mwenyewe. Mfano siwezi kutafuta kazi nje ya nchi. Imani potofu inakuwa
kama ni kipingamizi kinacho kukatisha tama juu ya jambo Fulani amabalo unataka
kulifanya. Ni muhimu kuepuka Imani potofu na kujua zaidi kuhusu imani hizo kama
kweli unashauku ya kufanikiwa katika maisha yako. Imani potofu sio tu kuwa
kipingamizi kwako pia inaangamiza maisha yako.
Vichocheo
vya nje
Namna unavyo fikiria inamfanya mtu asadiki kwamba
kila kitu kinatokea ni kwa matokeo ya vichocheo vya ndani na nje. Watu ambao
hawajafanikiwa wana External locus control kama unataka mafanikio jifunze namna
unavyo fikiria kutoka External locus control kwenda Internal locus control manake
una amini kila kitu kinachotokea katika maisha yako unauwezo wa kuzuia kitokee
au kisitokee.
Kutokuwa
na msimamo
Watu ambao hawafanikiwi katika maisha yao ni wale
wasio kuwa na msimamo au wepesi wakuvunyika moyo katika jambo fulani au
shughuri fulani. Hutakiwi kukata tamaa hata kama haufaulu jambo moja unatakiwa
kurudia mara kwa mara mpaka ufanikiwe.
Kutokubadilika
Husipo kuwa tayari kubadilika kutokana na mazingira
ya sehemu husika itakuwa ngumu kufanikiwa katika maisha yako. Maana itakushinda
kufanya kitu kingine kama cha kwanza kitakushinda. Jinsi utakavyo kuwa mwepesi
wa kubadilika kutokana na hali utakayo kutana nao ndio jinsi utaweza kumudu
maisha yako. Hukiwa mzito kudadilika ndivyo utakavyo shindwa kufanikiwa.
Kutokuwa
na mpango mkakati
Mpango ni muhimu katika mafanikio yeyote yale. Kama
hauna malengo au mpango utakao kuongoza hatua gani uzifuate ilikufikia lengo
lako itakuwa ngumu sana kupata mafanikio hayo uliyojiwekea katika maisha
yako.
Kutojiamini
Kama haujiamini na kuwa na aibu itakuwa ni vigumu
kutoa mawazo yako na kukata tamaa juu ya ndoto zako kama mtu akikuambia jambo
lako halitafanikiwa. Utakuwa unaogopa na kupata mashaka na hata kupuuzia nafasi
zitakazo kupeleka kwenye mafanikio. Kama unataka kuongeza nafasi ya kufanikiwa inakubidi
uwe na hali ya kujiamini katika kijambo unalotaka kulifanya.
Upungufu
wa rasilimali
Watu wangine wanakata tama kwa sababu hawana
rasilimali za kutosha. Kama kweli unataka kufanikiwa utafanikiwa bila hata kuwa
na rasilimali nyingi kwa hiyo usivunjike moyo. Unaweza kufanikiwa kwa
rasilimali ndogo hizo ulizo nazo. Mfano unataka kufanya biashara wenye mtaji wa
Tshs 1,000,000 na wewe una 500,000 unaweza anzisha biashara yako kwa hiyo
500,000 baadae mtaji ukikua utakuwa unaongeza mpaka itafikia huo mtaji ulio
tarajia kufikia. Usivunyike moyo kama unaupungufu wa rasilimali.
Uwoga/
hofu
Uwoga utakufanya ushindwe kufikia malengo yako.
Utakuwa unaogopa kufanya mambo yako kwa kuhofia watu au kuhofia kutofanikiwa
kwa jambo hilo. Kwa hiyo uwoga wako ndio kikwazo chako kitakacho kuzuia kufikia
malengo na mwisho wa siku utashindwa kufikia mafanikio uliyotarajia kupata.
Hukiepuka kuwa na tabia tajwa hapo juu basi
mafanikio yatakuwa mkononi mwako. Kuwa makini kwa kila jambo unalotaka kufanya
.
0 comments: