Leo tunaangalia baadhi ya mambo
ambayo yaweza kukusaidia kuepuka kuzini nje ya ndoa yako au kutoweza kumsaliti
mpenzi wako.
1.
Kujiepusha kuwa karibu na jinsi zingine ukiwa umelewa
Hapa nitoe ufafanuzi wa jambo moja
la jinsi ambapo nazungumzia masuala ya maumbile ambapo wengi wetu tunachanganya
neno jinsi na Jinsia.
Kuepuka kuwa karibu na jinsi tofauti
nawe ni suala gumu sana lakini ni vema unapokuwa unakula maji(kilevi) ni vema
ukawa makini kuwa mbali na mtu wa jinsi nyingine ili kuepukam kupata vishawishi
na kumsaliti mwenzi wako.
2.
Epuka mazungumzo ya kimahaba
Ni njia rahisi sana inayoshawishi
watu wengi kujiingiza kwenye usaliti ama mapenzi mapya ambapo endapo hautakuwa
makini na kujiingiza katika mazungumzo ya kimahaba na mtu wa jinsi nyingine
unaweza kujikuta unajiingiza katika usaliti wa kimapenzi lakini nji hii licha
ya kuwa ni njia moja wapo ya kuepuka usaliti ni njia nzuri ya kuanzisha mapenzi
mahusiano mapya ambapo wengi hushawishika na kujikuta kutamani kupata vitu
vipya katika mahaba ambavyo mtu aliyenaye kwa muda huo amevigusa katika
mazungumzo yao.
3.Kuwa mkweli
Ukweli ni jambo muhimu katika
kudumisha mahusiano na kuepuka usaliti kwasababu mwenzi wako anaweza kuhisi
kitu kuwa umeanzisha mahusiano na mtu mwingine ambaye mara kadhaa mnafanya nae
utani, hivyo ni vema ukawa mkweli kwa mwenzi wako kumweleza kuwa mtu huyo
mnafanya masihara nae na wala hakuna jambo lolote linaloendelea kimahusiano
tofauti na kutumia lugha kama ‘’Kwani unafikiri mimi nafanya nini nae’’ hilo
jibu sahihi katika kuboresha mahusiano yenu.
4.Epuka kupigana busu na jinsi
nyingine
Kumpiga busu mtu ambaye si jinsi moja
nawe ni kichocheo cha usaliti katika ndoa na hata mapenzi ya kawaida kwasababu
Mungu aliumba miili yetu katika misisimuko ya aina mbalimbali ambapo mtu
mwingine ukimpiga busu bila kujalisha kuwa ni mwanaume au mwanamke hujikuta
anasisimuka vibaya sana na kuhisi kuwa angekuwa sitakwa sita nawe kwa muda huo
angesisimuka hivyo si vema kufanya hicyo.
5. Usimweleze mtu hisia zako
Epuka kueleza hisia zako za kimahaba
kwa mtu asiye wa jinsi yako kwa mfano mtu kagombana na mpenzi wake ama mke/mume
wake si vema ukamwambia hisia zako kwake za kutomtenda bali ni vema kumwambia
kuwa siyo vizuri kugombana na mwenzi wake na jaribu kutoa ushauri ambao hauna
ushawishi wa kumwondoa kwa mwenzi wake.
Hapa sielezi kuwa haupaswi kuwa
mkarimu kwa watu la hasha bali nazungumzia kuwa makini na kuepuka kuwa mmoja wa
watu wenye historia za kuvunja mahusiano ya watu bali ukiwa mshauri mwema
utaheshimika zaidi.
6. Onyesha wajibu wako
Ni vema katika mahusiano kila upande
ukaonesha wajibu wake kwa mwenza wake ambapo waweza kumtia moyo mwenzi wako
kuwa yeye amekuwa sumaku kwako kwa kukupa faraja na hasa ni
mwanamke/Mwanaume ambaye ulikuwa ukitamani siku nyimgi kuwa naye na
hatimaye Mungu kakupa macho ya rohoni kumpata yeye.
Hapa wapo baadhi ya watu ambao si
wakweli ambao wanafanya maigizo kutamka maneno kama haya huku wakitoa zawadi
ili kuficha mambo yao huo ni usaliti na hapa nasema kuwa haifai….kama upo hivyo
jirekebishe acha usaliti.
nimeipenda hii blog.....ipo relevant in diverse ways.
ReplyDeletenimeipenda hii blog.....ipo relevant in diverse ways.
ReplyDelete