Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Hatua (5) za kuongeza tija kwenye kazi

Business people working together in an office


Natumaini utakuwa mwenye nguvu, afya njema na mchangamfu, leo nataka nikujuzi mambo haya yatakayo kuongezea  tija katika kazi zako na maisha yako kiujumla. Kanuni moja na nzuri ya  kuongeza tija katika kufanikisha au kupata matokeo makubwa ni hii

  Kanuni hiyo itakusaidia kusonga mbele kimaendeleo na kuongeza ufanisi wa kazi zako, kuwa na faraja kwa kitu unachofanya huchochea uwajibikaji na uhodari wa utendaji wako kazi. Ndio maana kujua nini unapenda kufanya ni muhimu sana kwenye mafanikio kwa kuwa faraja hutia mbolea ya matumaini na hukupelekea wewe kutaka kutenda mambo makubwa zaidi na mazuri katika kazi unayoifanya.

Zingatia mambo haya
1. Kuwa na sababu nyingi za kutopata mafanikio kutakufanya ukwame na kudumaza utendaji    wa     kazi zako. Epuka kuwa na visingizio vingi vya kutokuwa mtendaji mzuri wa kazi zako.
2. Huwezi pata matokeo mapya na mazuri ikiwa utaendelea kufanya maamuuzi  ya zamani. Kila siku kuwa na mawazo mapya na mbinu mpya za kukujenga na kuongeza ufahamu wako wa kazi unayoifanya.

3.  Kama bado hufurahii kazi ya mikono yako au kazi unazofanya basi ndoto zako bado ni ndogo. Utakapotafuta au kujishughulisha na kugundua umepata kazi nzuri unayoipenda ni mwanzo mzuri wa kutafuta mambo mengi zaidi ya maisha yako kama vipaji vyako, uzuri wako na uwezo wako wa kufanya mambo makubwa zaidi.
4.   Watu wenye mafankio huwekeza mara 10 zaidi kwenye kujifunza na kutafuta maarifa ya kujiendeleza na kujikuza kimaarifa na hiyo ndiyo siri kubwa ya kufanya kazi vizuri na kwa ubora. Ujuzi wa kazi ni zana kubwa ya maendeleo ya kazi yako, jifunze kila unapopata nafasi kwa manufaa yako ya hapo baadae.

5. Weka msimamo katika kazi yako kwa kufuatilia kitu kimoja mpaka umalize na kushika kingine. Jambo nzuri hufanikiwa kwa ustahimilivu wa utendaji wa kazi mpaka mwisho, usianze kitu na kuacha labda uwe na sababu ya msingi.


Toa maoni yako hapa..






0 comments: