Mada
yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila kinga
basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.
Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji
mimba, utupaji wa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani
yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine
zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga.
Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko
hiyo iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25
kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35)
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida
yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi.
NAMNA YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya
kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi
unaofuata, kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 December basi hiyo ndio
siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika
mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama
atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini
akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?
Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa24 hadi 48 baada
ya kujamiiana hivyo kama utafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado
litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.
Toa maoni yako..
0 comments: