Kama upo kwenye mahusiano basi hii itakuwa inakuhusu hizi ni
Hatua kuu zinazoonyesha penzi limepoteza muelekeo ni kama zifuatazo:-
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
Mapenzi na sawa na jani la mti. Huendelea kuwa na
mawasiliano na shina kwa kusaidiana na matawi. Ila siku ikifika jani
linadondoka. Hii utokea pale jani linapochoka na maisha ya kujishikiza. Haya
ndiyo sawa yalio kwetu binadamu. Mwanzo uanza kwa kasi zaidi na mwisho hufifia
kwa mawasiliano. Mtu anaweza kukata mawasiliano kwa sababu zake binafsi
zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale
walio mbali, mfano masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili
hadi mwisho wa siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa swali
kwanini husema nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa walio kwenye ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo.
Kama alikuwa anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa. Muda
mwingine kila mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha kila mtu
kivyake.
Hii hua na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na
mpenzi mwingine. Yule ambaye ulidhani umemchagua anakuja kuwa sumu kwako.
Unapenda umwone yeye ataki. Unapenda umpe zawadi yeye ataki, unapenda kutoka
naye out yeye ataki, na pale anaposema uwasiliane naye basi roho huweka
pembeni. Utagundua kuwa kama analazimishwa aongee.
Ikifikia sehemu hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza
jitihada za kutaka kuwa naye, wasio na imani hufikia mahali wanasema
nitaendelea kukaa bila kuoa. Kauli hii ni udanganyifu tu. Akisahau yale
yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume mwingine. Unapoona hali hii imeanza
jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake sana. Na pale unavyoona hali ni mbaya
zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu ambaye humwamini kwa kila jambo.
Au unaweza kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio
chako na mwisho wa siku utaona mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa
wanandoa itapotakiwa kufanya hili.
Kwa wanandoa ni muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao
wanaaminika na kukubalika na jamii. Ikishindikana basi waende katika ofisi ya
kata au ustawi wa jamii kwa msaada zaidi.
2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
Ni hali ya kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi
kuongea na wewe. Sababu kubwa anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi
unakuwa na asili ya mkunjo kwa wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na asili
na makunyanzi. Hapo ujue kuwa hali ni mbaya sana. Hapo hata ukimsesha anaona
kama unajisumbua tuu. Na kama ataamua kusema ni kidogo tu na mwisho inaedelea
kukaa kimwa.
Pia hata majibu yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na
sauti ya chini isiyo na mvuto au ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama
hapa jalibu kumnunulia zawadi mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi
wangu….nakupenda sana…….leo umependeza namna hii….. Kweli mimi nimechagua mke
mzuri au mme mzuri sana……kwani najivunia sana kukuona na kuwa na wewe muda
wote.
Wakati mwingine unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha
vyombo na hata kumwambia mkaoge pamoja. Utaona jinsi anavyoanza kubadilika
mpenzi wako. Hapa hakuna mchawi bali ni namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali
hii haiwezi kwisha ghafla kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa siki
hali inajirudia. Kwa hali ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22. Uendelea
kumwambia maneno yenye baraka na busara bila ya kukata tama. Uwe na imanii ya
hali ya juu kwani majibu utayokutana nayo si ya kawaida, lakini mwisho wa siku
hali itarudi kuwa ya kawaida kabisa.
3. HASIRA ZA
MARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende
mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo
watu huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake
amamsaliti. Mfano wa majibu utayokutana nayo ni kama haya:-
- mbona hivi mpenzi?
- mimi nifanyaje?
Wewe yanakuhusu nini?
Umepata hasara gani mimi kufanya hivi?
Fanya utakavyo?
Mimi ndo kila kitu?
- kwa nini yamefikia hapo?
- we ujui?
Hizi ni baadhi ya changamoto utazokutana nazo wakati wa
maojiano yako na mpenzi wako. Usimpige kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali
ikizidi kuwa ni kelele tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli
zingine. Utavyorudi atashindwa anzie wapi.
Kama ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya hivi:-
kaa kimya kwa muda, atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia mmeo
chakula cha kutosha na kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe maneno
matamu mkiwa kitandani na kujaribu kumgusagusa sehemu mbalimbali za mwili. Hapa
mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa kumuomba
msamaha. Hata kumpigia magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa hali hile
upendezwi nayo. Ni ya bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida na siku
nyingi kupita anza kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale mme wangu
kosa lilikuwa lako. Kama muelewa ataweza kijirekebisha ipasavyo na mwisho wa
siku mukarudi kama siku ya kwanza kuanza penzi lenu.
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
Hii ni hatua ya nne ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya
juu. Mpenzi wako hutamuona mchungu kupita kiasi. Hutaona kama kuna watu
wanamfundisha kuongea maneno haya. Ukweli ni kwamba ukishaona mke wako mara
nyingi yeye na wenzake, hana muda wa kukaa akuandalie chakula (kwa mwanamke
aliye kwenye ndoa) basi ujue kwamba rafiki zake wamemfundisha na ujue kuna
jambo linaendelea ambolo mwisho wake ni kutengana.
Kwa mchumba basi utaona maneno ya ovyo ovyo ili mradi
umwambie sasa mimi na wewe basi. Atafanya kila aina awezavyo utengane. Hii
huweza kuwa mwanaumme ndio kisa au mke mwenyewe ndio kisa. Akishindwa hapa
anaamua kuchukuwa maamuzi magumu sana ambayo hutasahau tena maishani. Kama vile
kumpigia mpenzi wake mpya na kuanza kuongea naye.
Hiyo atakuwa amekuheshimu, anamkumbatia na kumkiss ili mradi
uhuzunike kwa hili kasha mtenge ili awe huru. Hali hii huwa ni mbaya zaidi kama
mtu umependa. Hhiki ni sawa na wanavyofanya wanaume walio wengi katika uchumba
na doa. Ukimuuliza namba hii uliyosevu Juma mbona inaonyesha ni hile ya Asha
atakuambia ni rafiki yangu.
Ukiendelea kumbana atakuambia ni ya mke wangu. Sasa wewe
unasemaje au unataka nini? Haya utokea kwa wote wenye ndoa zao na wale walio
kwenye uchumba bila kujali mme au mke au mchumba.Haya ndiyo yanayojili sehemu
hii iwapo utashindwa kutatua hizo hatua tatu za mwanzo.
Namna ya kutatua sehemu hii ni kutumia zile njia elekezi ya
hatua ya kwanza. Kubwa zaidi hapa ni kuomba msamaha kwa kile kinachovumilika,
na kile ambacho akivumiliki ni kwenda kwa washauri nasaha kama vile maafisa
ustawi wa jamii kwa manufaa ya wote. Wao watakusaidia vizuri hata kama uko peke
yako na mwenza wako alikataa kwenda huko. Utamsahau na kuiona dunia ni tamu
zaidi y asana na utasema mwenyewe ulichelewa wapi kipindi yanatokea haya.
5. KUDAI KUTENGANA
Kama mnavyojua, mti uota, ukua, utengeneza majani, huishi na
hatimae mwisho kufa. Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata
kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke uende mbali ambako hutamwona
tena. Hapa hakuna jinsi, hata mahakama huamua kutenganisha ndoa kama walioana.
Hapa usipofanya kama atakavyo mpenzi wako unaweza kuishia hata gerezani au
kuchukua uamuzi wa kumpiga.
Kweli inauma sana kumwona mke/mme au mchumba
unaempendaanataka mutengane. Wengine huamua kujinyonga, wengine kunywa sumu,
wengine wanaamia baa na kuweka makazi yao. Mmoja hakikataa hakuna jinsi, mwache
aende kwa usalama.
Jinsi ya kutatua hili ni kwamba unapaswa kwenda kukubali
tatizo lililotokea. Kwani kinachotokea kwa wenzako hata wewe ipo siku
yatatokea. Katika maisha ya binadamu kuna kupenda na kutendwa, hivyo kutengana
ni moja ya sehemu ya maisha. Jaribu kutembelea sehemu zenye mkusanyiko wa watu.
Lakini usinywe pombe, na kama ulikuwa unakunya unaweza kuacha kabisa hatakwa
miezi kadha na usitembelee sehemu za pombe.
Unaweza kwenda disco na sehemu nyinginezo mzuri kama vile
kwenye mpira, kucheza puru, drafti, bao na hata karata. Hali yako itarudi kama
zamani. Utajiona wa kawaida (hii ni kama kwa mwanaume). Ukikutana naye usimwone
kama ni adui ako mkubwa, kwani yaliyotokea ni majaribu ya dunia. Na pale mkaapo
kwa muda mrefu na kuona kuna umuhimu wa kurudiana basi murudiane kwa moya
mmoja.
Kwa wanawake huchukua muda mrefu kama tendo lilifanywa na
mwanaume. Na tatizo lenyewe kama kumfumania mme au mchumba wake wakiwa katika
chumba kile kile anacholala yeye. Huwa anaona ni unyama. Kwa hili, mke huyu
kurudiana naye itachukua muda mwingi kwani lile swala humrudia mara kwa mara.
Na kama alimpenda sana bwana wake huamua usikuone kamwe.
Lakini hakuna jambo lisilo na mwisho. Mme unapaswa kwenda
kuomba msamaha kwa yule mke wako uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni
jambo la kawaida, kwani ile icha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii,
fanya hivi zaidi ya mara tano hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea
huruma na hatimae kuwa naye pamoja.
0 comments: