Wanadamu
wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi
vyema katika ulimwengu huu. kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu
ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia
mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao
wamebahatika.
Hakuna
watu waliozaliwa na bahati au mikosi, wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili
vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. yapo mambo kadha wa kadha ambayo
inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha
mazuri.
Umakini na
nidhamu. nidhamu
inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. hakikisha unakuwa na
ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila
siku. hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na
kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi
mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.
Dhamira. uaminifu umekuwa adimu sana kwa
watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa
kufanya ubadhilifu. ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri
zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.watu
waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo
zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako
na kufanya heshima yako ipotee. kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima
kuliko kuijenga.
Usiwe na
matumizi yasiyo na msingi.
watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda
waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. hakuna haja ya kutafuta sifa
mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya.
weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji
wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi
maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo
ulipo.
Fanya kazi
kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. uvivu wa kufikiri na wa kufanya
kazi unakwamisha maendeleo. tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi
kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi
ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. tuache ubishoo wakuona kuwa kuna
kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.
Kuwa
mbunifu, lakini
pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu
wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako.
mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza
Mungu utafanikiwa tu.
0 comments: