JE, WEWE huona
kwamba huna pesa za kutosha? Ikiwa ungeweza kupata pesa zaidi, labda ungenunua
kitu fulani unachotamani sana. Kama tu ungekuwa na mshahara mkubwa, ungeweza
kununua viatu unavyohitaji.Nyakati nyingine marafiki zako wanakuomba kwenda
kwenye burudani zinazohitaji pesa nyingi.
Badala ya
kuhangaikia pesa ambazo huna, mbona usijifunze kupanga matumizi ya pesa ulizo
nazo? Unaweza kungoja mpaka utakapoanza kujitegemea ndipo ujifunze jinsi ya
kutumia pesa. Lakini jiulize, Je, ungeruka kutoka katika ndege kabla ya
kujifunza kutumia parachuti? Ni kweli kwamba huenda mtu akafaulu kuifungua huku akibingirika-bingirika kutoka
juu. Hata hivyo, ingalikuwa afadhali kama nini ikiwa angalijifunza kanuni za
msingi za kutumia parachuti kabla ya kuruka nje!
Vivyo hivyo, wakati
bora zaidi wa kujifunza kutumia pesa ni wakati ungali nyumbani, kabla
hujakabili maamuzi mazito ya kiuchumi. Mfalme Sulemani aliandika: “Pesa ni
ulinzi.” Lakini pesa zitakulinda ikiwa tu unajua kuzitumia kwa hekima. Kufanya
hivyo kutakupa uhakika na kufanya wazazi wako wakuheshimu hata zaidi.
Jifunze Mambo ya
Msingi
Umewahi kuwaomba
wazazi wako wakueleze mambo yanayohusika katika kutunza familia yenu? Kwa
mfano, je, unajua inagharimu pesa ngapi kulipia stima na maji kila mwezi au bei
ya petroli, chakula, au kodi ya nyumba? Kumbuka kwamba unafaidika na huduma
hizo—na utakapoondoka nyumbani, wewe ndiwe
utakayelipia gharama hizo. Kwa hiyo, ni vizuri kukadiria gharama zako zitakuwa
kiasi gani. Waombe wazazi wako wakuonyeshe baadhi ya bili zinazoonyesha gharama
za huduma au bidhaa mbalimbali za nyumbani, na usikilize kwa makini jinsi
wanavyopanga bajeti, yaani, matumizi ya pesa.
Kutambua Magumu
Huenda ikaonekana
kuwa rahisi kutumia pesa vizuri, hasa ikiwa unaishi nyumbani na unapewa pesa za
matumizi au unapata mshahara. Kwa nini? Kwa kuwa huenda wazazi wako
wanalipia karibu kila kitu. Kwa hiyo, huenda ukaona kwamba una pesa
nyingi za kutumia upendavyo. Na kuzitumia ni raha.
Hata hivyo, tatizo
linaweza kutokea vijana wenzako wakikusukuma utumie pesa nyingi kupita
ulivyopanga. Ellena, mwenye umri wa miaka 21, anasema: “Baadhi ya vijana
wenzangu huona kwenda madukani kuwa tafrija. Na ikiwa hutanunua chochote,
hakuna haja ya kwenda.”
Hakuna mtu anayetaka
kutenda tofauti na rafiki zake. Lakini jiulize, ‘Je, ninapokuwa na rafiki
zangu, ninatumia pesa kwa sababu ninazo
au kwa sababu ninalazimika?’
Wengi hutumia pesa ili ‘kujitengenezea jina’ wanapokuwa na marafiki. Wanajaribu
kuvutia watu kwa vitu walivyo navyo badala ya utu wao. Hilo linaweza kukuletea
matatizo makubwa ya kiuchumi, hasa ikiwa una kadi ya mkopo. Unaweza kuepuka
jinsi gani matatizo hayo?
Dhibiti Matumizi
Badala ya kuponda
pesa zote na kumaliza kiwango kilichowekwa cha kadi ya mkopo au kuponda
mshahara wako wote kwa siku moja. Unapoenda matembezi na marafiki zako panga
mapema na kuamua kiasi utakachotumia. Mshahara wako weka katika akaunti yako ya
benki natoa tu kiasi ninachohitaji wakati huo. Pia ni vizuri kwenda madukani na
marafiki ambao hawatumii pesa ovyovyo na ambao watanitia moyo kulinganisha bei
katika maduka mbalimbali badala ya kununua vitu bila mpango.”
Huenda unafikiri
kwamba tayari unajua kutumia pesa zako vizuri. Lakini jiulize: ‘Nilitumia pesa
ngapi mwezi uliopita? Nilinunua nini?’ Umesahau? Basi, kabla mambo hayajaenda
mrama, chukua hatua zinazofuata.
1. Weka rekodi. Kwa mwezi mmoja hivi, andika kiasi
cha pesa ulizopokea na tarehe uliyozipokea. Andika kila kitu ambacho umenunua
na bei yake. Mwishoni mwa mwezi, jumlisha kiasi cha pesa ulizopokea na kiasi
cha pesa ulizotumia.
2. Panga bajeti. Katika safu ya kwanza, andika mapato
yote unayotazamia mwezi huo. Katika safu ya pili, orodhesha jinsi unavyopanga
kutumia pesa zako; ukitumia rekodi iliyo katika hatua ya kwanza. Kadiri mwezi
unavyosonga, andika kwenye safu ya tatu kiasi hususa ulichotumia kwa kila moja
ya mambo uliyopanga. Pia, andika gharama zote ambazo hukupanga.
3. Badili mazoea yako. Ukiona kwamba unatumia pesa nyingi
kuliko ulizopanga katika bidhaa fulani na madeni yanazidi kuongezeka, badili
mazoea yako ya kutumia pesa. Lipa madeni yako. Dhibiti matumizi yako.
Pesa zina faida
zinapotumiwa vizuri. Katika nchi nyingi maisha yanaweza kuwa magumu sana ikiwa
huwezi kuchuma na kupanga vizuri matumizi ya pesa.
0 comments: