Kitendo cha Ukeketaji kwa Wanawake tafiti zinaonesha kwamba
ktk nchi za Kiafrika, inakadiriwa kwamba zaidi ya nchi 25 zilikuwa zinaendelea
na Mila hii ya kukeketa wanawake.
Hali hii imeonekana pia ktk nchi za Ulaya na Amerika
ambapo ilikuwa inakadiriwa zaidi ya Wanawake Millioni 100 walikeketwa, na
Vijana wa Kike Millioni 2 walionekana kufanyiwa vitendo hivi kila mwaka, kwa
sababu mbalimbali za kidini, ngono, kijamii na usafi kwa mwanamke
Maana ya Neno Ukeketaji:
Ukeketaji ni Kitendo cha Kuondoa au Kukata Kisehemu au
Sehemu ya Uke (Kinembe/Kisimi au mashavu) cha Mwanamke kinachofanywa na
Mtu/Ngaliba ktk jamii ambaye hajapata mafunzo rasmi, na mara nyingi hutumia
vifaa visivyo takaswa na hakuna ganzi yeyote inayotumika.
Kitendo hicho huonekana kama sehemu ya Tohara kwa
Wanawake.
Aina mbalimbali za Ukeketaji
Kwa ujumla kuna aina tatu (3) za Ukeketaji ambazo
zimeonekana kufanywa;
I. Kuondolewa
kwa ngozi inayozunguka Kisimi/Kinembe.
II. Kukata
sehemu yote ya Kisimi
III. Kuondolewa/kukatwa
sehemu yote ya kisimi na Mashavu yote ya uke.
Sababu za Kukeketa:
i. Ni
imani za Dini kwa baadhi ya jamii
ii. Ngono
– Kuboresha tendo la kujamiana kabla ya ndoa kwa imani ya baadhi ya Makabila.
iii. Kijamii
– Kinadhihirisha ujasiri, kupevuka na kwamba sasa anaweza kuolewa ili kuleta
heshima ktk familia.
iv. Usafi
– Jamii ina imani kwamba Mwanamke asiyekeketwa huwa na Uchafu, hivyo kitendo
cha kukeketwa humuweka kuwa msafi na kuonekana kuwa maridadi.
Madhara ya Ukeketaji Wanawake:
Kiafya kuna madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa
vitendo vya ukeketaji wa wanawake kama;
Ø Kuzimia
Ø Kutokwa
na Damu nyingi
Ø Kupata
uambukizo (Infection)
Ø Kuambukizwa
VVU
Ø Kuambukizwa
homa ya manjano (Hepatitis B)
Ø Maumivu
makali Kidonda kutopona mapema
Ø Kuoza
kwa jeraha
Ø Kupata
Tetanus
Ø Maumivu
ya Kisaikolojia
Ø Kutofurahia
tendo la kujamiana kiufasaha
Ø Maumivu
wakati wa kukojoa
Ø Kuziba
kwa njia ya mkojo
Ø Kuchanika
vibaya wakati wa kujifungua
Ø Kuchelewa
kujifungua
Ø Kifo
Wajibu wa Jamii ktk Kupiga Vita Vitendo vya Ukeketaji:
• Kukemea
na kupiga marufuku vitendo na mila ya ukeketaji wanawake.
• Kuelimisha
wanajamii kuhusu Athari za Ukeketaji kwa wanawake.
• Kuhakikisha
sheria inachukuliwa dhidi ya yeyote atakaejihusisha na vitendo hivi vya
ukatili.
• Kuweka
Mkakati endelevu kutoa elimu ktk jamii
• Kuwashirikisha
Wadau ktk mikutano na habari hususani Viongozi wa dini, serikali, wanasiasa,
NGOs mbalimbali za kijamii.
Ili kupunguza na hatimaye
kuwaondolea vijana wa kike katika tatizo ili, kila kiongozi wa serikala, Dini
na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika ngazi zote anapaswa Kutetea sera za
kutokomeza hii mila inayotayarisha majina ya huyu motto wa kike.
0 comments: