Wakati mwingine mafanikio huhitaji kufanya kazi ngumu zenye kuchosha, lakini watu wasiokuwa na uwezo wa kufanikiwa wanapoletewa mambo mawili huwa wepesi zaidi kuchagua jepesi kulifanya.
Kama ni kazi, basi zisiwe
ngumu sana ziwe nyepesi nyepesi ambazo watazifanya bila jasho. Watu wasiokuwa
kwenye njia ya mafanikio hawapendi kujituma, wepesi kuchoka na mara nyingi
hupenda sana kufanya kazi kidogo na kulala sana.
Tabia za watu wasioweza kufanikiwa huwa ni za kukwepa kuwajibika. Hata kama kuna mtu anataka kumpatia kitu na akamwambia awahi kesho yake asubuhi, huchelewa kwa vile hawezi kujihimu asubuhi na kuacha raha ya usingizi, wakati mwingine hata akiambiwa asubiri mpaka muda fulani huwa hayuko tayari kusubiri.

0 comments: