Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Wanasaikolojia wanatuambia, Tumezaliwa na aina Mbili tu za Hofu.. Soma hapa Upate kujua Aina Hizo za Hofu..!!!

beauty and fear
Adui yetu mkubwa katika maisha ya leo, labda kuliko maadui wengine wote unaowafahamu ni hofu.Tuna hofu ya kupoteza kazi, hofu ya kuugua, hofu ya kufa, hofu ya kupoteza mpenzi, hofu ya kuanzisha biashara yako au labda hata hofu ya kukuza biashara yako, hofu ya kukosa mitaji n.k, kwa ujumla tuna hofu za aina nyingi zinazotuzunguka kila siku.

Na ni ukweli tu kwamba ni hofu hizo zinazofanya tusiwe wabunifu, tushindwe kujaribu mambo mapya, na labda ya hatari kidogo na tuendelee kuwa masikini, ni kwa sababu ya hofu zetu tunapoteza fursa nyingi.

Katika aina zote za hofu ninazo zifahamu, ni aina moja ambayo kwangu naona ndio kikwazo zaidi katika maendeleo yetu. Hofu ya kushindwa.Tuna hofu kwamba nikianzisha biashara ikafa watanicheka, nikijaribu kuuza kipaji changu (labda cha kucheza mpira au uchekeshaji) labda wenzangu wataona mimi si bora kuliko walionitangulia.

Ni kwa sababu hiyo basi tunashindwa kabla hata ya kuanza,tunakosa ubunifu na jamii inakosa vionjo mbalimbali kutokana na vipaji mbalimbali tulivyonavyo.
Zaidi sana dunia inakosa ladha ya kipekee, inayotokana na upishi wako wa kipekee, kumbuka wewe ni wa kipekee, na hivyo hivyo fikra zako, kipaji chako, mtazamo wako na hata utendaji wako. 

Niliwahi kusoma mahali ambapo mwandishi alijenga hoja kwamba Mungu alituumba, pamoja na mambo mengine, tumsimulie hadithi, na kwamba Mungu anapenda hadithi,kwahiyo tafadhali acha woga,utengeneze hadithi,utusimulie na sisi pia, kabla hujapewa nafasi ya kufanya hivyo kwa huyo aliye na nguvu kuliko vyote.


Vilevile, habari ambayo labda si njema sana kwako ni kwamba kushindwa/kufeli ni jambo unaloweza kuliepuka tu, kama alivyosema mwanafalsafa mmoja,kwa kutofanya chochote,kutojaribu chochote,kutosema chochote na kutokuwa chochote.

Lakini wanasaikolojia wanatuambia, tumezaliwa na aina mbili tu za hofu nazo kama zifuatazo; 

1) hofu ya kuanguka(fear of falling)
2) hofu ya kelele/sauti(fear of noise),

hofu zingine zote tumefundishwa na ama wazazi wetu au walimu wetu shuleni. Ushauri wangu ni kwamba huu ni wakati wa kufuta hofu hizi zingine zote ambazo si asili yetu, haswa ukizingatia kwamba sisi si wototo tena,na kwa kweli inafaa kujifunza kutoka kwa watoto(labda niseme kujikumbusha, labda tumesahau,siku moja tuliwahi kuwa watoto),wao wanaujasiri wa kujaribu chochote bila kujali wengine watawafikiriaje au watawaonaje,au matokeo yatakuwaje.

Leo ni wakati wa kuzika hofu zako, na kuishi kama ulivyo katika uhalisia wako (as a real you), jiulize tu kama usingekuwa na hofu yoyote ungefanya nini tofauti leo, halafu amka nenda kakifanye, haijalishi kama ni kuanza biashara ya kuuza mbogamboga, au kufungua kituo cha kulea watoto (day care), au kufungua biashara ya kuuza vitu kupitia intaneti, au kuandika vitabu n.k chochote unachoweza kufikiria,nenda kafanye,tutafurahi kusikia hadithi yako.Kitu pekee cha kuhofia ni hofu yenyewe.



0 comments: