Images
Kumlazimisha Mtu Ampende Asiyempenda ni Sawa na kuingilia uhuru wa Mtu na Furaha ya Moyo wake.. Habari kamili iko hapa..!!!
Tatizo ambalo limekuwa sugu na
linalochangia watu kushindwa kuelewana na kuwa na mifarakano ndani ya ndoa au
uhusiano, ni wanafamilia.
Mara nyingi mwanamume au mwanamke
ambaye anavunja uhusiano ghafla bila maelezo yoyote, wengi huamini ni
kukosekana kwa upendo wa kweli kwa mmoja wao, lakini uchunguzi wangu wa ndani
ambao nina uhakika nao kwa asilimia mia na hata wewe utaniunga mkono ni kwamba,
tatizo kubwa la mifarakano ya ndoa ni hilo ambalo nimelitaja hapo juu. Najua
wengine wataniona kama mpiga ramli.
Adui mkubwa wa uhusiano wa
wanandoa au wapenzi ni baadhi ya wanafamilia, sichagui ni nani bali wao
wanajijua. Hii hutokana na mpenzi wako kutokuwa chaguo lao, kama utakuwa na
msimamo wa kukataa wazo lao la kutafuta mwingine, lazima watakutishia
kukutenga.
Suluhu yao ni kuachana na mpenzi wako ili uwe na yule ambao wao wamemchagua
japo si chaguo lako. Familia imekuwa sumu kubwa kwenye uhusiano mwingi kwa
kuingilia matakwa kwa kutumia uwezo wao kuwatenganisha na kukulazimisha kutoa
uamuzi wa mdomoni na si wa moyoni kumkataa umpendaye.
Wengi huwa tunaamini uamuzi wa
mtu kuvunja penzi ghafla ni pindi anapokosa mapenzi ya kweli, lakini
ukichunguza kiundani utakuta uamuzi wa mhusika kuvunja uhusiano si wake bali ni
wa wanafamilia.
Kwa walio na msimamo hutengwa na
familia hata wazazi hufikia kumtolea radhi. Napenda kurudia, huwezi kuusemea
moyo wa mwenzako. Nafasi ya kupenda ni ya mhusika na si mtu wa pembeni au
wazazi.
Hata ndugu bado hawana nafasi ya
kuingilia uamuzi wa mtu, hata mkiwa mmemzidi umri. Mkiona mwenzenu amejenga
ninyi mnatakiwa kuongeza uimara na si kila siku kutafuta njia za kuvunja
uhusiano huo.
Kumbuka kumlazimisha mtu ampende
asiyempenda ni sawa na kuingilia uhuru wa mtu wa utashi na furaha ya moyo wake.
Siku zote uzito wa mzigo aujuae aliyeubeba si mtazamaji.
0 comments: