Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Historia fupi ya Mapinduzi ya Zanzibar



Zanzibar ni maarufu katika historia ya vita vifupi. Vita vya karne ya 19 ambavyo vilimalizika kwa kiasi cha dakika 45 lakini vimetumika kuonyesha mara zote ukatili kabla ya utawala wa ukoloni wa Ulaya Afrika Mashariki.
Kitu ambacho kinajulikana kwa uchache kabisa ni  kumbukumbu ya karne ya 20, ambapo Zanzibar ilishuhudia mfano wa vita vifupi kabisa vya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika Mapinduzi haya, Serikali ilidumu zaidi ya karne ilipinduliwa si chini ya siku moja. Taifa huru jipya la Zanzibar la jamii ya kisultani inayojumuisha waarabu, wahindi, waswahili, wangazija na wenyeji ikiongozwa na mrithi wa Sultani lilipotea kwa haraka ya ajabu.
Usiku huo ulitawaliwa na hali ya wasiwasi, kushangaza, ushupavu na kukata tamaa. Usiku huo ulianza saa tisa usiku. Kabla ya siku kuu kubwa ya kidini . Siku kuu hii iliwashajiisha makundi makubwa ya watu kukusanyika kuzunguka mji mkongwe. Watu walijenga mahema au kulala chini ya minazi huku wakisubiri ufunguaji wa sherehe wakati wa asubuhi. Baadhi ya makundi ya watu yalikuwa ni makundi ya vijana, baadhi ya vijana hawa walikuwa ni wafuasi wa mwanasiasa aliyejulikana kwa jina la John Okello.  Suali la wafuasi wangapi walimfuata Okello katika mapinduzi hili ni suali la kutatanisha.


 Kwa hakika mwishoni mwa siku hiyo maelfu ya watu walijiunga na mapinduzi hayo baada ya kujulikana matokeo. Ni kweli kwamba, inasemekana kwamba Jemedari Mkuu Okello alikuwa na askari bataliani nne dhidi ya majeshi ya serikali usiku huo wa mapinduzi, lakini Jee, walikuwa watu wangapi wanapohisabiwa?
  Okello aliarifu kwamba mapinduzi yalianza usiku wa manane pale alipoachana na askari mia mbili na khamsini wa batalioni yake ya nne kwenye kambi ya Polisi ya Ziwani na ghala ya silaha.   Saa tisa usiku alimrisha watu wake kukata waya wa ngome ya ziwani.

Hilo lilikuwa tendo la mwanzo halisi la Kimapinduzi na lilisaidia kuwajua washiriki halisi wa Kimapinduzi. ("Separate the men from the boys").  Okello aliarifu juu ya watu wake wakati huo".  Ukubwa wa kikwazo chetu ulikuwa wazi kwao.  Tulikuwa tumejizatiti kwa mapanga, mikuki na vyuma vya magari na ulikuwa tunabahatisha kupambana uso kwa uso na askari waliosheheni bunduki za rashasha...." Wote waliondoka au kukataa kutambaa kupitia kwenye waya isipokuwa watu arubaini tu. 
Watu arubaini hawa ndio walioikamata Zanzibar na kuuangusha utawala wa Kisultani na zaidi ya miaka mia moja na thalathini na tatu kupitia  masultani 12.
  Wanamapinduzi hawa walitambaa kiasi cha mita 25 ndani ya kambi ya Ziwani.  Ndani walikuwepo maishirini ya maaskari.  Askari hawa kama walivyo watu wengi wenye busara Zanzibar walikuwa wamelala ghorofa ya juu ambayo pepo baridi za bahari ziliweza kupoza/kuburudisha misitu ya joto.  Askari wawili tu walikuwa macho na walikuwa wanashika zamu ya ulinzi chini.
  John Okello na askari wake waliwavamia walinzi hawa.  Bunduki za rashasha zililia na watatu kati ya askari batalioni ya nne waliuliwa.  Juu ya hivyo mmoja wa walinzi pia aliuawa, alimalizwa na mshale uliolengwa na Mwana Mapinduzi aliyeitwa Albert.  Hapo tena Okello alikuwa uso kwa uso na mlinzi aliyebakia, ilikuwa hapa ndipo utabiri wa ushindi wa Mapinduzi ulipatikana.  Watu hawa wawili walitwangana, Jemedari Mkuu anatwambia hivi"  Nilimpokonya  bunduki, tulipigana na kufanikiwa kumpiga tako la bunduki shavuni"  Upigaji risasi ulisimama.  Watu wa  Jemedari Mkuu walikuwa tayari wamefika kwenye malango ya chumba  cha silaha ambamo mamia ya Silaha za kisasa na maelfu ya risasi na baruti zilikuwa zimefungiwa. 
Askari wasiokuwa na silaha waliokuwa ghorofa ya juu, walijaribu kuteremka chini kwa fujo kwa kutumia ngazi moja tu ya nje huku wakiwa wamejaa wasiwasi.  (kwa kudhibiti hali ya amani na utulivu ya kawaida, silaha zote hufungiwa kwa ajili ya kuzihifadhi wakati maofisa  wa Polisi wanapokuwa hawapo kazini).  Askari wa batalioni ya nne ya Okello walivurumisha mvua ya mikuki, mishale na mawe kwa askari walioduvaa na askari hawa wa  Serikali walilundikana wenyewe katika ngazi nyembamba.  Bunduki aliyoihodhi Okello ambayo ilikuwa na risasi tatu ilitumika kulengea risasi.  Polisi hawa walirudi ghorofa  ya juu kutafuta kamba ya kushukia kwa kupitia dirishani.
  Ilikuwa tayari wamechelewa, milango ya Chumba cha kuhifadhia silaha ilikuwa imevunjwa na Batalioni ya lnne walivamia ndani.  Mara tu kila mmoja alikuwa yatari amesheheni bundundi ya rashasha.  Wapiganiaji uhuru  hawa ambao walianza usiku kwa silaha za vyuma vya magari zilizochongwa, sasa walikuwa ni jeshi lilsheheni silaha nzuri na bora.  Askari hawa waliwasha moto wa ndege kwenye vyumba vya ghorofa ya juu na mara tu polisi waliobakia walisalimu amri.
  Askari wa Sultani walijaribu kujilinda vikali dhidi ya waasi hawa.  Kikosi cha askari maalum chenye gari zenye kasi cha kukamata wahalifu kiliwasili kiasi cha saa baada ya ngome ya ziwani kukamatwa na wanamapinduzi.  Askari hawa 75 walikuwa na bunduki nyepesi na walikuwa hawalingani na batalioni iliyosheheni silaha na iliyojidhatiti ndani ya ngome ya silaha.  Waasisi waliachia askari wa Sultani kukaribia na baadae kuwa vurumishia mvua ya risasi.  Mashambulizi yalikuwa makali sana hadi vichaka vya karibu vilishika  moto, Polisi wa Sultani walirudi nyuma huku wakiwa wamekata tamaa.
  Kwa kutumia  kituo chao hiki kipya, wanamapinduzi walitawanya bunduki  kwa batalioni nyengine tatu (ambazo tayari zilikuwa zimeshazizunguka sehemu muhimu lakini bado kuzishambulia.  Kwa amri ya mara moja vituo vyengine vya Polisi na mawasiliano vilishambuli na kukamatwa.  Upinzani mkubwa ulikuwa kituo cha Polisi cha Malindi, ambapo hadi asubuhi lmilio ya risasi ilisikika.
 Lakini juu ya hivyo hadi mchana Sultani alikuwa ameshakimbia  nchi, iliyobakia ni historia tu.

WAZANZIBARI MAARUFU

SITI BINTI SADI.
Akiwa Nyota wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab tokea miaka ya mwanzo ya santuri, Siti aliweza kuifanya Taarab kuwa maarufu kutokana na muziki wake mtamu na nyimbo za mapenzi zilizobeba ujumbe wa nguvu za kijamii na uchambuzi wakisiasa. Jambo moja lililoifanya kazi yake kuwa ya kiharakati ni vile kuimba kwake kwa kutumia lugha ya watu wa kawaida. Baada ya kuishi kwa muda mrefu katika mitaa ya Ng’ambo mjini Zanzibar, baadaye Siti alitembelea nchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki akiimba na kuuza rekodi zake. Lililompa umaarufu zaidi miongoni mwa watu ilikuwa ni muziki mpya uliorekodiwa katika lugha yao wenyewe. Baada ya wasomo wanadai kuwa rekodi hizi za zamani zilichangia sana kuieneza lugha ya Kiswahili.

Akiwa mtoto wa watumwa, Siti alianza maisha kwa akali ya kitu, lakini kwa juhudi yake mwenyewe na sauti yake ya ajabu, aliweza kwanza kuimba taarabu ya kawaida, baadaye katika makasri na kumsifu Mfalme, na hata kuimba kwa Kiarabu. Baadaye aliigeuza midundo na mifumo ile ya kishairi na kuwa katika vinanda vya kawaida. Matokeo yake, Taarab ya Kiswahili ilimfanya awe Nyota na yeye kuifanya taarab iwe aina ya sanaa ambayo bado ni maarufu visiwani na isiyokosekana katika harusi na sherehe zote za Kizanzibari ..

BARGHASH BIN SAID
Huyu ni Mfalme wa Tatu wa Zanzibar, aliyetawala kuanzia mwaka 1870 mpaka 1888. Mama yake alikuwa mtumwa (aliyewachwa huru kwa kuzaliwa yeye), Sultani wengi wa Zanzibar walikuwa watoto wa wanawake watumwa. Baba yake, Seyyid Said bin Sultan, alikuwa mfalme mlowezi wa Sultan wa mwanzo wa Zanzibar. Barghash anasifika kwa ujenzi wa miundo mbinu ya Mji Mkongwe, ikiwemo maji ya bomba, vituo vya polisi, barabara, bustani, hospitali na majumba mengi ya kiutawala kama vile Beit el Ajaib.

Pengine alikuwa Sultan wa mwisho kuweka kipimo cha uhuru wa kweli dhidi ya udhibiti wa Wazungu. Alishauriana na “Washauri” kadhaa wa kizungu ambao walikuwa na ushawishi mkubwa, lakini alibaki kuwa mtu imara waliyepambana naye kumdhibiti alipambana na wanadiplomasia kutoka Uingereza, America, Ujerumani, Ufaransa na Ureno na mara kwa mara aliweza kuiangusha kitaalau nchi moja baada ya nyengine katika kinyang’anyiro cha kabla ya Ukoloni. Ni mtoto wake, Khalid, ambaye katika    mchuano wa kurithi ufalme, alishindwa katika Vita vifupi kabisa katika histora.

SHEIKH ABDALLA SALEH FARSY
Alikuwa ni mfano wa karne ya Ishirini, katika safu ndefu ya Ulamaa wa Kiislam kutoka Zanzibar. Mchango wake maarufu katika uislamu ni kuchapisha QUR’AN TAKATIFU, yenye kurasa 807, ambayo ni tafsiri ya mwanzo kamili inayokubalika katika lugha ya Kiswahili Sheikh Abdulla Saleh Farsy vile vile alikuwa kabobea katika sarufi ya Kiarabu. Akiwa katika umri wa miaka ya ishirini, alikuwa anaandika mashairi kwa kiarabu, jambo linaashiria ukubwa wa kiwango cha elimu ambacho ulamaa wa Zanzibar walikuwa wanasambaza nyakati zile.

Sheikh Abdulla aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa shule za msingi za Unguja na Pemba mnamo mwaka 1949, Mkuu wa Shule ya Lugha ya Kiarabu mwaka 1957 na Kadhi Mkuu wa Zanzibar mwak 1960. Aliondoka visiwani baada ya Mapinduzi ya 1964 na akafia Omani Novemba 9 mwaka 1982.

TARIA TOPAN
Mfanya biashara, “mwana mfalme” wa kihafidhina, ambaye alijipatia utajiri wa mailioni kutokana na biashara ya karafuu na mamilioni mengine zaidi wakati alipokuwa anafanyakazi kama mkusanyaji Ushuru wa Forodha katika bandari ya Unguja na Pemba. Katika dhamana ile, alitakiwa kumlipa Sultani kiwango kikubwa kisichobadilika cha ada kila mwisho wa mwaka, kutokana na fursa aliyopata kwa kuteuliwa mkusanyaji mapato. Alipiga mahesabu na kuona kuwa angeliweza kukusanya pesa nyingi zaidi kuliko zile ambazo angelilipa, kama ikiwa biashara ingekwenda vyema. Na kwa wakati ule, biashara Zanzibar ilikuwa nzuri. Bei ya karafuu na viungo vyengine ilikuwa juu, mahitaji yalikuwa makubwa na bidhaa za viwandani ambayo vitu hivi zilifanyiwa biashara zilionyesha kushuka kupungua kila mwaka, kwa vile vitendea kazi na mbinu za kutendea kazi vilikuwa rahisi katika nchi za Magharibi.

Kwa utajiri wake huu, Topan aligeuka kuwa mfadhili Mkuu wa mji. Aliweka Wakfu na kujenga Kituo cha Afya kilichonakishiwa ambacho kipo Kaskazini kabisa mwa Bandari ya Mji Mkongwe. Vile vile alitoa “Wakf” vikataa vya ardhi vilivyokusudiwa kuwanufaisha wazee wasiojiweza.

NAHODHA “SMITH WA ZANZIBAR”
Yeye hakuwa Mzanzibari, lakini alikuwa rafiki wa mwanzo wa Kimarekani kuja Zanzibar. Alifanya biashara kwa mapana katika mwambao wa Afrika Mashariki kwenye miaka ya 1800. Akiwa mfanyabaishara kutoka Salem, Massachussets, aligundua kitu kilichomuunganisha na wafanyabiashara wa Zanzibar ambao Utajiri wao ulitokana na mfanya biashara mwerevu na wa kuaminika. Pamoja na manahodha wafanya biashara hawa, alifanyanao mapatano ya bei na kuweza kuwa marafiki haraka sana.

Wamarekani wao waliuza nguo za pamba (Mrekani) na kununua vipusa, viungo na sandarusi ambayo ilitumika kutengeneza vanishi kwenye viwanda vya New England. Kwa kufanya biashara na Marekani, kuliifanya Zanzibar kuwa kituo Kikuu cha Biashara katika maeneo haya.. Hata kufikia mwaka 1830, katika kipindi cha miezi 18, jumla ya vyombo 32 kutoka Amerika vilishatia nanga katika bandari ya Zanzibar.Mnamo mwaka 1836 kiwango cha biashara baina ya nchi mbili hizi ilihakikisha kuanzishwa Balozi za Amerika za kudumu katika Mji Mkongwe. William Smith alisafiri “kuzunguka pembe” ya Afrika mara nyingi katika safari ndefu za kutoka Amerika na visiwani kiasi cha kujulikana kama Smith wa Zanzibar katika pande zote za ikweta

0 comments: