Ndoa
yeyote inahitaji vitu vingi vya msingi ili iweze kudumu na iwe yenye furahaa na
upendo ndani yake. Leo tutatizama nguzo 3 muhimu katika ndoa nazo ni kama
zifuatavyo;
1. Utulivu
2. Mapenzi
3. Huruma
Utulivu huletwa na
mwanamke, na ndio maana ikatafsirika “ili mpate utulivu kwao”. Utulivu huzaa
mapenzi na huruma baina ya wanandoa, kwa maana nyingine, mwammke ana nafasi
kubwa ya kujenga au kubomoa ndoa, hii haina maana kuwa mwanamume hana nafasi ya
uharibifu, bali nafasi ya mwanzo inachukuliwa na mwanamke bila ya upinzani.
Kwa hekima za mungu
amewaumba wanawake tofauti kabisa na wanaume kimaumbile (Physical), kihisia
(emotional), na kinafsi (Psychological), hii yote ni kwa ajili ya wadhifa na
majukumu yao katika jamii.
Hivyo basi, sababu
kubwa ya wanandoa kuchokana, au kuzeeka kwa ndoa kunasababishwa na mwanamke,
pale ambapo atashindwa kutumia nafasi yake na vipawa alivyopewa kuleta utulivu
katika ndoa yao, na hapa nitajaribu kujadili baadhi ya visababishi
vinavyopelekea kuzeeka kwa ndoa au kuchokana visababishi ambavyo huwa
vinadharaulika na kuonekana vitu vidogo vidogo hususan kwa wanawake wengi.
a) Kuzoeana:
kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu
mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususan kwa upande wa
mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu
ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.
Matatizo
mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo,
ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano: siku za
utoto wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo
anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula
unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata
kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.
Lakini
baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la
kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi
utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi
anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato,
kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani.
Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.
b) Mazungumzo:
Mazungumzo ni njia muhimu ya kujenga ndoa na kuiimarisha, aidha ni njia ya
mkato ya kuchokana na kuchukiana. Mwanamke ambaye hajui wakati gani aseme nini
na wakati gani asiseme, hujikuta katika wakati mgumu ndani ya ndoa yake.
Kwa
mfano: Mwanamke ambaye kila anapoongea na mume wake huanza mazungumzo yake na
matatizo na lawama humfanya mumewe awe na woga kila anaposikia sauti yake, na
kuiona nyumba chungu, kwa sababu hakuna binadamu anayependa kusikia matatizo tu
wakati wote.
Mwanamke
wa aina hii huwa anamsubiri mumewe kwa hamu kubwa, na anapofika tu na kabla
hata ya kupata rizki, anaanza kumsomea orodha ya matatizo; watoto wamerudishwa
shule, karo haijalipwa, shangazi yako amepiga simu mjomba kalazwa Hospitali na
kadhalika na kadhalika. Nyumba ya aina hii huzeeka haraka na wanandoa
kuchokana.
c) Kusomana Tabia:
ni udhaifu mkubwa kwa wanandoa ambao wana mwaka mmoja katika ndoa yao wakawa
bado hawajasomana tabia, au wakawa wameishasomana tabia, lakini kila mmoja
akawa anataka tabia zake ndio ziwe dira.
Kwa
mwanamke mwenye busara na mwenye kuithamini ndoa yake, husoma tabia za mumewe
na kuangalia jinsi gani anavyoweza kuzioanisha na zile zake ili kuepusha
migongano, aidha hutafuta fursa muafaka ya kumkinaisha mumewe juu ya fikra
fulani au tabia fulani ambayo yeye haridhiki nayo.
Ni
muhimu kwa mwanaume vilevile kuzisoma tabia za mke wake, vitu gani vinamuudhi,
na vitu gani vinamfurahisha
0 comments: