Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika
kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na
jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na
uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa
kitaasisi na kifedha
1.
Mradi
huo unaitwaje?, Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni
kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na kipindi
cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
2.
Maswali
mengine ni kama ifuatavyo; Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni
ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo
lilianza nkwa nani?
3.
Kwanini
tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki?, Je, mradi ni suluhisho halisi
na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu
utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
4.
Unaweza kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje
katika jamii hii.
5.
Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili
kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia
utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?
6.
Malengo au Lengo kuu la mradi ninini? Madhumuni yake mengine ni yapi? Shughuli
za mradi na majukumu madogomadogo ninini? Ambayo lazima yapangwe kimantiki na
kwa matarajio yenye kufikia lengo.
7.
Ni wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu, mchango wa
wadau hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu ?
8.
Kuna uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala la
mazingira linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na magonjwa
yasiyotibika yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa mradi huu?
9.
Umepanga kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi huu?
Uendelevu wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu kwa namna gani?
10.
Swali linguine ni kama kuna mradi kama huu uliowahi kutekelezwa hapo au jirani
na hapo katika kipindi kifupi kilichopita.
NB: Maswali haya yakijibiwa vizuri kwa mtiririko
sahihi huitwa andiko la mradi na ifuatayo ndio mpangilio wa jumla ambao
wahisani wengi wameupenda katika kuandika andiko la mradi.
0 comments: