Ikiwa
mmoja wao ana matatizo, ama mume
au mke inabidi wote wawili waende kwa daktari aliyebobea katika masuala hayo. Huenda ikawa
ama mume au mke ana matatizo ya kutoweza kumtosheleza mwenziwe. Mara nyengine
wote wawili au mmoja wao anaweza kutibiwa na kupona, hivyo kuwa sawa kabisa na
hali yake kutulia. Mara nyengine hubidi upasuaji ili kuweza kurekebisha kasoro
hiyo kati yao.
Ikiwa hali
ya mmoja wao au wote wawili itarekebishika basi wataendelea kuishi kama mume na
mke. Ikiwa tatizo hilo halikurekebishika basi zipo hali kadhaa ambazo zinaweza
kujitokeza. Miongoni mwazo ni:
1. Wote wawili wana shida kwa sababu ya maumbile yao, hivyo
kutoweza kutimiza mahitaji ya kimapenzi. Hapa itategemea, kwani kila mmoja
anaweza kuridhika na hali hiyo bila kunung’unika. Katika uamuzi wao sheria
haitawaingilia nao wanaweza kuishi pamoja bila ya shida yoyote.
2. Kama mwenye tatizo ni mwanaume, Mume ambaye
hawezi kumtosheleza mkewe kitandani ni sababu ya mke ama awe anatembea nje ili
kujitosheleza kimwili. Lakini hili ni jambo ambalo limekatazwa na kupigwa vita
na sheria. Hivyo, sheria ina kipengele cha kuwa mwanamke huyo anaweza kwenda
kushitaki na ana uwezo wa kumuachisha na
mumewe ili aweze kupata mume mwengine kuolewa na hivyo kuepukana na zinaa.
Lakini ikiwa mke ataamua kukaa na mumewe kwa sababu ya kuwa tatizo hili likuja
baadaye na kwa maslahi ya kuwatazama watoto, sheria haitamlazimisha kuachwa.
3. Kama mwenye tatizo ni mwanamke, Kwa
mwanamume itakuwa haina tatizo anaweza kukaa na mkewe hasa ikiwa wameishi kwa
muda na wana watoto na tatizo limekuja baadaye. Na hapo mume atakuwa na thawabu
kwa kumtazama mkewe katika hiyo.
Toa maoni yako
0 comments: