Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Mambo Tunayo yakosea tukiwa na Wapenzi wetu

sad black couple


Nazungumzia juu ya mambo ambayo yanaweza kuwa kero kwa mpenzi wako ama kwa kujua au kutokujua.

(1) USAFI WA CHUMBA
Linaweza lisionekane kama ni jambo kubwa na muhimu, lakini nataka kuwahakikishia kwamba, usafi wa chumba ni kati ya vitu muhimu sana vya kuzingatia kabla ya kuingia faragha na mwandani wako.
Hili ni jukumu la wanawake zaidi, lazima uhakikishe chumba kinakuwa kisafi, kuanzia mashuka na vitu vingine vilivyomo chumbani. Mpangilio mzuri wa chumba na usafi kwa ujumla vinamsogeza mwenzi wako karibu zaidi na tukio husika.

Chumba kinapokuwa kichafu, kina harufu mbaya kinapoteza ladha ya kile kinachotarajiwa kufanywa, hali ambayo inaweza kusababisha mafanikio ya kazi yenyewe kuwa madogo sana.

(2) PUPA
Kuna baadhi ya wanaume wana tabia ya kuwa na pupa uwanjani. Hii ni kero kubwa sana. Faragha inahitaji maandalizi, sasa unapoingia uwanjani bila ‘kupasha’ kwanza kwa mazoezi madogo madogo ni wazi timu lazima ifungwe!



(3) KUZUNGUMZIA MAKOSA
Unapoingia uwanjani halafu utake  kifanyike kikao cha usuluhishi juu ya mambo aliyokufanyia mpenzi wako, ni kosa. Kufanya hivyo, kunapunguza utayari kwa kazi mnayotarajia kuifanya.

(4) KUTAWALA
Kwa bahati mbaya sana, wanaume ndiyo wamekuwa na tatizo hili zaidi. Wanakuwa watalawa mchezoni, hawataki maelekezo, wanafanya vile wanavyoona inafaa. Baadhi yao hawataki wenzi wao waoneshe makeke.

Wengine huenda mbali zaidi, huwapiga marufuku wenzi wao wasijishughulishe kwa chochote na inapotokea wakifanya hivyo, huwajia juu wakidai kwamba ni wasaliti ndiyo maana wakawa wataalamu sana.

(5) UKALI
Rafiki zangu mapenzi ni burudani, sasa unapopeleka ukali katika eneo hilo unapoteza maana kabisa. Kuwa na lugha tamu, acha maneno makali. Ikitokea kuna mahali pakahitaji maelekezo basi yatoe kwa sauti ya mahaba zaidi na siyo kelele, lawama na sauti ya juu. Ukifanya hivyo unampotezea mwenzako msisiko na mwisho utakayokuwa umefanya yanakuwa kazi bure!

(6) KUDHARAU HISIA ZA MWENZIO
Suala la kusikiliza hisia za mwenzako si ombi, ni kanuni za mapenzi! Utakuta mwingine anakazana kumfanyia kitu fulani mpenzi wake, akiamini anamfurahisha, kumbe ni kinyume chake.
Ikiwa mpenzi wako amekueleza wazi kuwa unachokifanya hakimfurahishi, heshimu hisia zake na ufanye anachokipenda ili mkitoka uwanjani wote muwe mmeridhika.

(7) MANUKATO MAKALI
Kuna rafiki zangu baada ya kuoga usiku kabla ya kulala, hujipulizia manukato, jambo hili si sahihi. Unapokuwa faragha na mwenzi wako, epuka kujipulizia manukato hasa makali.
Inapendeza zaidi kama mkikutana katika eneo hilo, mkiwa na harufu zenu ‘natural’ zaidi kuliko kero ya manukato. Tatizo hili lipo kwa wanawake zaidi.

(8) KUMUACHA NJIANI
Hili ni tatizo kubwa na muhimu kuliko yote, hakuna aibu kama hii rafiki zangu. Kwa bahati mbaya, wengi huwa hawasemi, lakini madhara yake ni makubwa.
Si rahisi kueleza kila kitu hapa, lakini elewa kwamba kuanza safari pamoja na mwenzako, halafu njiani unamkimbia na kumuacha porini, ni tatizo kubwa sana katika uhusiano.
Rafiki zangu, nimejitahidi kuzungumza kwa lugha ambayo naamini wengi mnaelewa vyema, iwapo kuna sehemu imekutatiza na ungependa kupata mbinu na ufafanuzi zaidi, tafadhali tuwasiliane.


0 comments: