Ulishawahi kufanya kazi na mtu msumbufu? Watu
wasumbufu hukera sana pale ambapo unataka kufanya kazi zako nao wakakukwamisha
kwa namna moja au nyingine kwa makusudi au bila kukusudia.Watu hawa wanaweza
kukusumbua usiweze kufanya kazi zako kwa kukuingilia katika shughuli zako kwa
mambo mengine. Asimia kubwa ya watu wanaokwamisha kazi zako ndio hao hao
wanaochelewa kukamilisha mambo yao kulingana na ratiba, wanachelewa kwenye
mikutano au makazini na wale wasiotoa ushirikiano kazini kwa kutowajibika na
makosa wanayofanya.
Watu hawa huwezi kuwakwepa ila unaweza kutumia njia
ambazo zitawafanya wasikusumbue kwa
kiasi fulani na kuendelea kufanya kazi zako kama kawaida.
Tumia
njia hizi kuwamudu watu wasumbufu na wakwazaji.
1.Kuwa
mtulivu.
-Unapokwazika kwaajili ya mtu fulani, jitahidi
kutopandisha hasira lakini onyesha kuwa hujapendezwa na yeye kukukwamisha
kufanya kazi zako. Mtu huyu pia anaweza kukusumbua kwa kukuingilia katika mambo
yako pasipo ruhusa. Kufanya hivyo kutamfanya aweze kukusikiliza na kuwa mstaarabu
kwa lile utakalomwambia. Lakini vilevile kuwa kwako mtulivu utaepusha kugombana
au kupelekea nyinyi msivunje uhusiano wenu wa kikazi au kirafiki na kuwa
pamoja.
2.
Elewa dhamira yake.
-Naamini kila mtu anaweza kubadilika, hivyo kujua
kwanini mtu fulani anakukwaza sana katika shughuli zako kutakusidia kutambua
utakabiliana naye vipi au utamuelezeaje kuhusu kukukwaza kwake na kupelekea
yeye kubadilika kama inawezekana. Jaribu kujua kwanini anakuwa hivyo na kwanini
hataki kutoa ushirikiano wake kwako.
3.Mueleze
kuhusu anavyokukwaza.
-Utapomweleza kuwa yeye si muungwana itakusaidia
kuondoa kujilaumu kwanini hukumwambia ukweli kuhusu tabia yake lakini pia kwa
kumwambia utamfanya abadilike na kufanya mambo yako kuwa rahisi.
4.Pata
ushauri kutoka kwa watu wengine.
-Ongea na wanfanyakazi wenzako au rafiki zako kujua
mawazo yao kuhusu namna ya kuwamudu watu wasumbufu. Kwa kuwashirikisha wanaweza
kukupatia mbinu nzuri za wao walizotumia
katika kufanya kazi na watu wa namna hiyo. Jifunze kutoka kwao.
5.Wapuuze
au achana nao.
-Ninachomaanisha hapa ni kwamba unapokwazika
kwaajili ya watu wa namna hiyo puuza usumbufu wao kwa kutowapa nafasi ya
kuendeleza tabia zao. Kwa kuwapuuza watajiuliza wenyewe kwa yale wanayofanya
kuwa sio sahihi na kubadilika.
6.
Wasaidie watakapo hitaji msaada kutoka kwako.
-Licha ya kuwa wamekukwaza katika mambo mengi, kwa
kuwasaidia kuna uwezekano wa wao kubadilika kutokana na unavyowasaidia na
kujifunza kutoka kwako.
7.
Usichukulie usumbufu wao kama ni swala lako binafsi.
-Mara nyingi watu wa namna hiyo hukwaza pia na watu
wengine katika mambo yao. Ukichukulia kukukwaza kwao kibinafsi utaumia kwa
kuwaza kwanini wanakufanyia hivyo ni vyema uwaelewe na kuwaepuka kama
ikiwezekana ili usikwazike kwa kutofanya
shughuli zako za msingi kwaajili yao.
0 comments: