Kuonewa si
jambo dogo. Uchunguzi fulani nchini Uingereza unasema inaonekana kwamba zaidi
ya asilimia 40 ya ripoti katika vyombo vya habari vya kitaifa kuhusu vijana
wanaojiua zilisema kwamba kuonewa kulichangia sana kuwafanya wajiue.
Kuonewa
hutia ndani mengi kuliko kushambuliwa kimwili. Kunaweza pia kutia ndani mambo
yafuatayo.
Kushambuliwa
kwa maneno. “Wasichana wanaweza
kutumia maneno makali, Siwezi kusahau majina waliyonibandika au mambo
waliyosema. Walinifanya nijihisi sifai, sipendwi, na nihisi kuwa bure kabisa.
Afadhali wangenipiga badala ya kuniambia maneno hayo.
Kutengwa. “Wanafunzi walianza kuniepuka. Wangenizuia
nisiketi nao wakati wa chakula cha mchana kwa kuonyesha kana kwamba meza
imejaa. Kwa mwaka mzima, nililia sana na nilikula peke yangu.
Kupitia
Intaneti. “Kwa
kuandika mambo machache tu kwenye kompyuta, unaweza kumharibia mtu sifa
kabisa—au hata kuharibu maisha yake. Huenda ukafikiri ninatia chumvi, lakini
hilo linaweza kutokea!” Kumwonea mtu kwa njia hii kunatia ndani kutumia simu ya
mkononi kutuma picha au ujumbe mfupi wenye kudhuru.
Kwa nini watu huwaonea wenzao? Hizi ni baadhi ya sababu za kawaida.
Wao wamewahi
kuonewa. “Nilikuwa
nimechoshwa kwa sababu wenzangu walinitendea vibaya hivi kwamba nikaanza kuwaonea
wengine ili rafiki zangu wanipende. Baadaye nilitafakari na kutambua kwamba
lilikuwa kosa kubwa sana!
Wanaiga watu
wenye sifa mbaya. “Mara
nyingi vijana wanaowaonea wengine . . . wanawaiga wazazi, ndugu na dada zao
wakubwa, au watu wengine wa familia,
Wanajifanya
eti wana uhakika—lakini wana wasiwasi. “Watoto wanaowaonea wengine huonekana kana
kwamba wana ujasiri na uhakika lakini wao hufanya hivyo ili tu kuficha uchungu
na hisia za kwamba hawastahili.
Ni nani wanaoweza kuonewa kwa urahisi?
Wanaojitenga.
Vijana
fulani ambao hawajui kuchangamana na wenzao hujitenga na wengine na wanaweza
kuonewa kwa urahisi.
Vijana
wanaoonwa kuwa tofauti na wenzao. Huenda baadhi ya vijana wakaonewa hasa kwa sababu ya sura, rangi,
au dini au hata kwa sababu wana udhaifu fulani wa kimwili—jambo lolote ambalo
mwoneaji anaweza kutumia kuwadhihaki.
Vijana ambao
hawajiamini. Vijana
wanaowaonea wengine wanaweza kutambua mtu anayejidharau. Mara nyingi watu wa
aina hiyo ndio wanaoonewa kwa urahisi kwa kuwa si rahisi kwao kujitetea.
Unaweza kufanya nini unapoonewa?
Usionyeshe hisia zozote. “Waoneaji hutaka kujua ikiwa
wamefaulu kukuhuzunisha, Usipoonyesha kwamba wamefaulu, wanachoka na kuacha. Mwenye
hekima huituliza [roho yake] mpaka mwisho.
Usilipize
kisasi. Kulipiza
kutazidisha tatizo, hakutalitatua. Usilipize yeyote uovu kwa uovu.
Usijiingize
katika matatizo. Kwa
kadiri unayoweza, waepuke watu au hali ambazo unaweza kuonewa.
Toa jibu
lisilotazamiwa. Jibu,
linapokuwa la upole, hugeuza ghadhabu.
Tumia
ucheshi. Kwa mfano,
mwoneaji anaposema kwamba umenenepa kupita kiasi, lipuuze jambo hilo na useme:
“Inaonekana ninapaswa kupunguza kilo kadhaa!
Ondoka. “Kunyamaza kunaonyesha kwamba una
nguvu kuliko yule mtu anayekusumbua, Kufanya hivyo kunaonyesha unaweza
kujizuia—yule anayekuonea hana uwezo huo.
Jitahidi
kujiamini. “Watu
wanaowaonea wengine watatambua iwapo hujatulia, watahakikisha kwamba
wanakufanya usijiamini hata kidogo.
Mwambie mtu.
Kulingana na
uchunguzi mmoja, zaidi ya nusu ya watu wote walioonewa kwenye mtandao
hawakuripoti kilichowapata, labda kwa sababu ya kuaibika (hasa wavulana) au kwa
sababu waliogopa watadhulumiwa wakiripoti. Lakini kumbuka kwamba waoneaji
hufaulu zaidi jambo wanalofanya lisipofichuliwa.
Kufunua
kinachoendelea kunaweza kuwa hatua ya kwanza ya kukomesha hali ngumu
unayokabili.
0 comments: