Wengi hujiuliza ni kitu gani hasa mtu anachopaswa kuwa nacho
kusudi aweze kupata mafanikio hasa ya kiuchumi. Wengine hudhani mtu anatakiwa
awe na elimu kubwa sana ndipo aweze kufanikiwa, lakini siyo kweli, unaweza
ukawa na elimu kubwa tu hata hivyo hali yako kiuchumi bado ikawa siyo
nzuri.
Pia sina maana ukiwa na elimu kubwa huwezi kufanikiwa la hasha, wapo watu wengi tu na elimu zao wamepata mafanikio makubwao kiuchumi.
Pia sina maana ukiwa na elimu kubwa huwezi kufanikiwa la hasha, wapo watu wengi tu na elimu zao wamepata mafanikio makubwao kiuchumi.
Na unaweza ukafikiri pia labda ukifanya kazi kwa kutumia
nguvu nyingi sana huku ukilala masaa machache kwa siku labda utaweza
kupata mafanikio ya haraka kiuchumi lakini hilo nalo wataalamu wanakuambia
kwamba siyo kweli. Sasa ni nini hasa kinachotakiwa? Jibu ni kwamba, mtu
anapaswa kuwa na tabia za kijasiriamali. Tabia za kijasiriamali
zipo nyingi lakini hapa tutaizungumzia hii moja tu ambayo ni uvumilivu.
Uvumilivu ni ile hali ya kuendelea kufanya kazi kwa muda
mrefu ili kutimiza lengo ulilojiwekea pasipo kukaka tamaa haraka hata
ikiwa utapita muda mrefu kiasi gani. Watu wenye tabia hii, hufanya kila
linalowezekana katika kuhakikisha lengo walilojiwekea linatimia, huchagua lengo
moja.
Hawashiki mawili kwa wakati mmoja, hawachoki njiani na ni wabunifu, wanapoona mbinu ama mkakati fulani hauzai matunda basi hubadilisha na kutumia mbinu nyingine katika kuhakikisha tu lengo walilojiwekea limetimia. Hutumia muda wao mwingi kujifunza na kujaribu ujuzi/stadi mpya.

Mambo mengine unayopaswa kuwa nayo ni wazo zuri la
biashara. Biashara yaweza kuwa ni ya aina yeyote ilimradi inakidhi vigezo vya
kuwa biashara inayowezekana na kulipa vizuri. Dira na malengo yako ni lazima
pia uweze kuvibainisha waziwazi.
Ukiwa mvumilivu katika kila jambo lazima utafikia malengo
yako
ALLAH akubariki
ReplyDeleteALLAH akubariki
ReplyDeleteAsaneeee kwahiliii darasa
ReplyDeleteElimu bora kabisa
ReplyDeleteAsante nimekuelewa
ReplyDelete