1. Kufanya mazoezi ya
viungo.
Ni muhimu sana kufanya mazoezi hasa wakati wa asubuhi maana mazoezi
huchangamsha akili na kukuwezesha kufikiri kwa ufasaha zaidi. Pia mazoezi
yanaimarisha afya na afya njema ni muhimu sana kwako kufikia malengo yako.
2. Kupitia malengo na
mipango ya siku. Katika muda huu wa asubuhi pitia malengo uliyojiwekea maishani
na mipango mbalimbali ya kufikia malengo hayo. Pia weka mipango ya siku hiyo na
jinsi ya kuitekeleza. Katika saa hii unaweza kuangalia ni kwa kiasi gani
umefanikiwa ama umekaribia kuyafikia malengo yako.
3.
Kujihamasisha. Ni muhimu sana kujihamasisha kabla hujianza siku yako. Hii
itakusaidia kuweza kuimiliki siku yako na kuwa na mtizamo chanya juu ya maisha
yako na kazi zako. Unaweza kujihamasisha kwa kujisomea kitabu, kusikiliza
vitabu vilivyosomwa au kuangalia video mbalimbali za kuhamasisha.
0 comments: