Katika dunia ya sasa watu hununua mahitaji yao kwa kutumia pesa. Kama hawana njia za kupata pesa watakuwa maskini. Umasikini mbaya zaidi ni ule ambao unawafanya watu wasiweze kupata chakula. Kwa hali hiyo, wanakuwa dhaifu na wanaweza kufa kwa njaa. Hali nyingine ya umasikini ni ile ambayo watu wanaweza kuwa na chakula kiasi au kidogo lakini hawana maji salama, huduma za matibabu, nyumba au mavazi bora.
Takwimu za mwaka 1992 zinaonyesha kuwa karibu robo ya Watanzania wanaangukia katika kundi la kwanza la umasikini na nusu ya Watanzania wanaangukia katika kundi la pili. Katika mwaka 1995 karibu theluthi (1/3) ya idadi ya Watanzania walikuwa masikini. Hali hiyo huenda ni mbaya zaidi hivi sasa. Lakini umasikini una vipengele vingine zaidi licha ya kutokuwa na fedha za kutosha kununulia chakula, nguo, kujenga nyumba na kumudu gharama za matibabu. Utafiti kuhusu umasikini unaonyesha kuwa watu maskini zaidi:
|
|
Pata kujua aina mbili za umasikini unao tukabili katika maisha yetu ya kila siku, nazo ni kama zifuatazo;
Umasikini wa Mapato na Usio wa Mapato
Kwa kuwa kuna njia nyingi za kuzingatia suala la umasikini ni vyema kuwa na makubaliano ya fasili za umasikini. Fasili hizi zitasaidia katika majadiliano na katika kufanya mipango. Kutokana na tulivyosema hapo juu, ni vyema kufikiria juu ya umasikini kwa namna mbili:Umasikini ulio na kipato kidogo:
Kinafikiriwa kuwa wakati mapato ya watu ni chini ya dola moja kwa siku (kama shilingi 800/= za Tanzania). Hii ina maana kwamba hawatakuwa na chakula cha kutosha, uwezo wa kupata tiba, watakuwa na mavazi na nyumba duni.Umasikini Usio wa Kipato:
Kuna wakati watu wanakuwa na fedha kidogo na hivyo hawawezi kumudu shule nzuri au kuwa na maji salama. Watu wanaoishi katika umasikini usio na kipato wanategemewa kudumaa na kufa mapema. Aidha, watu wa aina hiyo hawategemewi kushirikishwa katika kutoa maamuzi yanayohusu maisha yao.
Kipato
cha kimasikini kinapima watu wana wananunua na kutumia pesa kwa kiasi gani.
Umasikini usio na kipato unahusu ubora wa maisha na maisha ya kijamii.
Unapima vitu vingi ambavyo vinawaondoa watu katika hali duni ya umasikini na
kuwaingiza katika hali bora. |
0 comments: