Images
Usikosehe haya ukakosa mke/mume!!
Maamuzi ya kuoa au kuolewa, si
maamuzi madogo, ni moja ya maamuzi makubwa ambayo vijana wengi wa kike na wa
kiume wana kutana nayo kila siku. Sasa katika kufanya maamuzi haya ukweli ni
kwamba sehemu kubwa ya vijana mpaka wafike mahali pa kumpata kijana au binti wa
kusema huyu ndiye haswa wa kuoa/kuolewa nae.
Lengo la waraka huu mfupi kwako
kijana mwenzangu ni kutaka kukueleza sababu kadhaa ambazo kupelekea vijana
wengi kufanya makosa katika kutafuta mwenzi wa maisha.
*Wengi wanakuwa tayari
wameshafanya maamuzi ya nani ataishi naye.
Vijana wengi
huwa wanaomba Mungu awape mtu sahihi wa kuishi naye na wakati huohuo tayari
kwenye nafsi yake anakuwa na mtu wake kwamba lazima huyu tu ndiye nitaishi
naye. Na kwa sababu hiyo ina kuwa ni vigumu kwao kumpata mtu wa mapenzi ya
Mungu na pia ina muwia kazi Mungu kukuonyesha mke au mme wa kusudi lake kwani
tayari umeshafanya maamzi ndani yako, je Mungu afanye nini kama sio kunyamaza.
*Maneno
ya kujitamkia
Kuna baadhi na hasa hapa ni akina dada kwa sababu mbalimbali kama vile kubakwa,
kujeruhiwa katika nafsi kwa sababu ya kuachwa na mchumba wake hufikia mahali
wakasema mimi sitaki tena kuolewa. Sasa inpofika muda umepita na wanataka tena
kuolewa wananaza kuomba Mungu awape mume, wakati huo wamesahau kwamba
walishatamka kwamba hawataki tena kuolewa. Nisikilize ukisema hutaki kuolewa au
kuoa tena, maana yake unaifunga nafsi yako hapo kwamba hutaoa /kuolewa.
*Dhambi.
Kuna baadhi ya vijana huwa wanakuwa awali kuna baadhi ya dhambi wamezifanya na
hawajazitubia, na bado wana taka mtu awaoe au wa kumwoa. Vitabu vya dini vipo
very clear kama kuna dhambi umeficha hutafanikiwa, sasa inategemeana, lakini
pia inahusiana sana na kutofanikiwa kwako pia kumpata hata mwenzi tu. Nikupe
mfano mara nyingi watu wanatoa mimba, au watoto wanaozaa, nao pia kupata mume
au mke huwa inakuwa kazi kweli kweli.
*Kutokuenenda
kwa Roho.
hii ni
pamoja na zoezi zima la kutafuta mke au mme. Sasa kwa sababu wewe unaenda kwa
mwili, mara eti nataka mtoto portable, mguu wa chupa, mweupeee, nk. Hivyo vitu
unavyotaka wewe kuna wengine pia wanataka hivyohivyo na matokeo yake mnaanza
kugombaniana msichana au mvulana kwa sababu tamaa za miili yetu zinawaongoza
huko.
*Kuwa na
vigezo binafsi.
Vijana wengi sana katika suala zima la kupata mke ua mme, ukweli wengi
wao wana vigezo vingi sana ambavyo kila mmoja angependa huyo mchumba wake awe
navyo. Utasikia lazima awe wa kabila ya kwangu, awe portable, mweupee, mrefu
ndio mzuri, ajue kutabasamu na kisha awe ana ulamba.
Sawa mi sikatai hivyo vigezo,
lakini nikuulize swali Je! Unayajua mawazo ya Mungu kuhusu wewe kwa habari ya
mkeo au mmeo? Je kidini hivyo vigezo vyako vinakubalika/ na je mke/mme mtu
huchagua mwenyewe au hupewa na Bwana?
*
Kufanya maamuzi kabla ya wakati.
kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu”.Hili
ni jambo la kawaida, hata wakati wa uchaguzi kura mtu harusiwi kupiga kama
hajafikisha miaka kumi na nane kwa nchi nyingi. Vivyo hivyo hata suala la
kutafuta mke au mume lina wakati wake maalumu.
Ukitaka kulifanya nje ya kipindi
ambacho Mungu amekipanga kwa ajili yako utateseka hadi uchoke. Kumbuka kila mtu
ana muda wake, hivyo basi hakuna muda maalumu wa kila mtu kuanza kutafuta mke
au mme, bali kila mtu ana muda wake na mara tu unapowadia Mungu humjulisha mtu
wake.
Nisikilize ukiulekeza moyo wako
upate kujua haya nisemayo na ukajizuia kufanya makosa kama haya, basi nataka
nikuhakikishe suala la kupata mke au mme wa kutoka kwa Bwana litakuwa ni jepesi
sana,ni sawa sawa na kuombea chakula na ukishafumbua macho ukaanza kula moja
kwa moja ukiwa na uhakika kimeponywa na kubarikiwa.
0 comments: