Images
Watu wengi huzani kuwa Harufu mbaya itokayo Ukeni ni matokeo ya Uchafu na kutojisafisha Vizuri. Soma hapa Kujua Jinsi ya Kujikinga Kutoa Harufu Mbaya
Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya
itokayo
ukeni ni matokeo ya uchafu na kutojisafisha vizuri.
Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio
ya kuondokana na tatizo hili. Kihalisi,
badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua.
Japokuwa
ni kweli mara nyingine inaweza
ikawa ni sababu ya uchafu.
Ila mimi naamini walio
wengi huwa wanazingatia usafi.
Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya
kujikinga
VISABABISHI
i. Bacteria
Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia
kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao
jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri.
Kutokana
na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia
sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake
kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha
tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna
hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na
kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.
ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni
mfano wa maziwa mgando(mtindi)
iii. Magonjwa ya
zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na
kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala
makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza
akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke
anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una
ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.
iv. Maambukizi
ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya
ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba
na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia.
Mara
nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu
yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa
mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya,
uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa
kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha
utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni
kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa
tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba
kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.
vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa
unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini
wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali
za kukata harufu zinaweza kukudhulu.
JINSI YA
KUJIKINGA
• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha
kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye
madhala.
• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap)
usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.
• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni
muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.
• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam
wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha.
Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali
za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.
• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama
tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.
0 comments: