Images
Epuka Ndoa yenu kwenda mara kwa mara kwa Wasululishi.!! Jifunze Unyenyekevu, Ukikosea kuwa wa kwanza kuomba Msamaha
MAPENZI ni furaha, lakini siyo
wote hubahatika kuwa katika furaha hiyo. Makosa fulani yakifanyika, ama kwa
kujua au kwa bahati mbaya huwa mwanzo wa kupoteza furaha katika mapenzi.
Kwa bahati mbaya sana, baada ya
kupoteza furaha ni vigumu kuirudisha kwa haraka, hata kama ulikuwa na mwenzi
mwingine kwa muda mrefu lakini baada ya kugundua matatizo yake na kuachana
naye, utapata shida sana kupata mwingine.
Lakini pia, hata kama utampata ni
vigumu sana kumzoea kwa muda mfupi, kuzoea mazingira na kujihakikishia kuwa
ndiye mwenzi wako wa kudumu.
Siyo ajabu sana wapenzi kuachana,
lakini inapotokea wewe unakuwa wa kuachwa kila siku, lazima ujue kwamba kuna
tatizo, tena tatizo lenyewe lazima litakuwa upande wako. Ni jambo gumu kidogo
kupata hekima ya kugundua jambo hili, lakini waliobahatika kupata wamekuwa
wakifanya maamuzi ambayo hayawaumizi mioyo yao.
Haya mambo yanawezekana rafiki
zangu. Kwanza ni kukubali kujifunza, kuangalia wapi ulikosea, ni kipindi gani
wenzi unaochana nao wanapatwa zaidi na hisia za kukuacha n.k. Baada ya hapo ni
rahisi kusogea mbele zaidi katika kujua jinsi ya kutatua tatizo ulilonalo.
Katika mada hii nazungumza zaidi na wanawake.
Wapo wanawake wengi sana ambao
wanahangaika kwa sababu ya kuachwa kila siku. Kila mwanaume anayekuwa naye,
baada ya muda mfupi tu, anaachana naye! Hajui tatizo, badala yake anaishia
kulia tu. Kulia kwako hakutakusaidia lolote kama hutakaa chini na kujiuliza ni
wapi kwenye matatizo, ni sehemu gani huwa unakosea!
Kujua chanzo cha tatizo ni mwanzo
mzuri sana wa kuelekea kwenye kupata ufumbuzi. Una miaka ishirini na nne tu,
lakini umeshakuwa na wanaume tisa! Hili ni tatizo, tena kubwa ambalo linahitaji
dawa ya kuponya na siyo ya kutuliza maumivu.
Sikia kilio hiki: “Mpaka sasa
nimechoka, nahisi kama sitakiwi kuwa na mpenzi, maana kila ninayekuwa naye
lazima ananiacha. Neno nakupenda halina thamani kabisa katika maisha yangu ya
sasa, yaani nimechanganyikiwa kabisa sijui nifanyaje niweze kupenda tena?”
Kilio kama hiki kipo kwa
wanawake wengi sana nchini, lakini kwa uchache sana ili tuweze kuepukana
maummivu pitia vipengele vifuatavyo:
ACHA KUJIRAHISISHA
Kwanza jaribu kujichunguza kama una tabia ya kujirahisisha. Ni kweli umekuwa na
tabia ya kujishusha thamani na kuona kama wewe ni wa kuonewa? Kuchezewa?
Mwanaume mwenye ndoto na mwanamke wa baadaye wa maisha yake (mke) hahitaji
mwanamke wa aina hii.
Anapenda zaidi awe na mwanamke
mwenye msimamo anayetambua thamani yake yeye mwenyewe na maisha yake kwa
ujumla. Hapendi mwanamke rahisi rahisi! Kama utakuwa wa aina hii, hata kama
atakuwa amekupenda, ataishia kukutumia na kukuacha, kwani wewe mwenyewe
umejionesha wa namna hiyo.
Mwanaume anapenda sana mwanamke wa
kumsumbua kidogo, angalau baadaye apate stori za kusimulia; “Lakini mama
nanilii ulinisumbua!”. Huu ni ukweli ambao baadhi ya watu wanaukwepa. Acha
kujirahisisha.
Kujirahisisha huku ni pamoja na
suala zima la kufanya mapenzi, usiwe na haraka na tendo hilo, usiulizie juu ya
kufanya mapenzi, lakini kama ikitokea jamaa akataka, usikubali haraka. Onyesha
msimamo wako, ukianisha usivyotaka kuchezewa. Hapo utaonekana mwanamke bora na
mwenye msimamo na si wale wasio na staha.
ANZA KUJICHUNGUZA
Wakati mwingine mambo yako yasiyotamanika yanaweza kuwa chanzo cha wewe kuachwa
na wenzi wako kila wakati. Angalia tabia zako, tizama mienendo yako, marafiki
zako, kauli zako na kila kitu ambacho unadhani kinaweza kuwa tatizo.
Mwanaume hapendi kuwa na mwanamke
ambaye ana kampani mbaya, kwani anaamini na wewe pia inawezekana ukawa na tabia
chafu kama rafiki zako, lakini kauli nzuri kwa mwenzi pia ni kati ya mambo
ambayo mwanaume mwenye nia ya kuoa atavutiwa navyo. Jiangalie upya!
UNYENYEKEVU/KUJALI
Kujiona wewe ni bora kuliko wanawake wote hakukusaidii, sana sana kunazidi
kukurudisha kwenye matatizo yale yale kila siku. Mwanamke ambaye hajali na
haonyeshi umakini wowote wakati akizungumza na mpenzi wake, hana sifa ya kuwa
mke.
Kama ni kweli unataka kuwa mke,
lazima uwe makini, uonyeshe kujali kwako na kumuona mwenzi wako kila kitu
kwako. Mheshimu, mpe nafasi ya kwanza, hiyo inaweza kuwa safari nzuri sana ya
kuelekea kwenye mafanikio.
Jifunze unyenyekevu, ukikosea
kuwa wa kwanza kuomba msamaha, kubali kusamehe na hakikisha kwamba unakubali
kufundishwa unapokosea. Usiwe mtu usiyejali, ambaye upo tayari kwa lolote, hata
kama ni kuachana na mwenzi wako. Hii ni kati ya sumu hatari zitakazokufanya
uishie kuachika kila siku.
0 comments: