Images
Ni kawaida kwa Binadamu kuwa na Hofu pale anapofanya jambo lolote kwa mara ya kwanza, Pata Habari Kamili Hapa Jinsi ya Kuondoa Hofu Hiyo
Ni kawaida kwa binadamu kuwa na
hofu pale anapofanya jambo lolote kwa mara ya kwanza. Yaweza kuwa ni mara yako
ya kwanza kwenda shule ( labda darasa la kwanza, kidato cha kwanza au mwaka wa
kwanza chuo kikuu).
Lakini vilevile inawezekana ni mara ya kwanza kuanzisha biashara, au ni mara
yako ya kwanza kuoa au kuolewa au ni mara yako ya kwanza kusafiri kwa ndege au
meli,au labda ni mara yako ya kwanza kuchangia katika mjadala fulani,mara ya
kwanza kuajiriwa au kujiajiri au pia inawezekana ni mara yako ya kwanza kufanya
mapitio(review) ya makala kama hii na kutoa maoni yako.
vyovyote vile itakavyokuwa(kuna
mifano mingi unaweza kuifikiria), ukweli ni kwamba aghalabu kuna shauku au hofu
inayoambatana na kufanya jambo lolote kwa mara ya kwanza.Lakini ni ukweli
vilevile kwamba hofu au shauku hii inakuwa kubwa zaidi pale ambapo jambo
lenyewe linapokuwa geni si kwako tu peke yako, bali kwa jamaa au ndugu au
marafiki walio karibu yako,
mathalani kama katika jamaa au
ndugu au rafiki zako wa karibu hakuna aliyewahi kupanda ndege,basi inapotokea
wewe ukapata nafasi ya kupanda ndege,hakika shauku yako itakuwa kubwa zaidi,
maana hujui masikini kitatokea nini utakapokuwa ndani ya ndege.
Hujui kama ukisikia joto ndege
ikiwa angani, ufungue dirisha au ufanye nini,hujui kama kutakuwa na wakati wa
kuchimba dawa njiani au itakuwaje,bahati mbaya maswali yote haya hakuna
yeyote kati ya jamaa zako anayeweza kukupa majibu,mpaka pale wewe mwenyewe
utakapo ingia kwenye ndege.
Jambo moja la kuzingatia ni
kwamba, huwezi kuahirisha safari eti kwa sababu hujui nini kitatokea
njiani,jambo lingine la faraja ni kwamba pamoja na hofu,vilevile kuna furaha
na burudani ya aina yake inayotokana na kufanya jambo fulani kwa mara
ya kwanza,na niseme tu kwamba hii peke yake ni sababu tosha ya kukufanya wewe
ujaribu jambo fulani kwa mara ya kwanza.
Kutokana na nadharia hii,tunaweza
kufikia hitimisho kwamba,burudani au furaha hupatikana katika [au baada
ya] hofu,au shauku na kwa kweli hata maumivu.
Basi kama kuna jambo hujawahi
kufanya; labda hujawahi kupanda mlima kilimanjaro[kama mimi], au hujawahi kuona
simba[au kusikia akinguruma] hatua chache kutoka ulipo au hujawahi kuona
maajabu mengine yaliyopo huko duniani[na yapo mengi] hakikisha unapata
nafasi hiyo.Labda hujawahi kufanya biashara jaribu leo,
labda tangu kuzaliwa hujawahi
kutoa hotuba au kuongea mbele za watu tafuta nafasi ufanye hivyo.kama
nilivyokwisha kukuasa,mambo haya si kweli kwamba yatakuwa rahisi mara ya
kwanza,hakika mara nyingi yataambatana na hofu na maumivu kiasi,lakini hatimaye
mambo haya huleta furaha na burudani ya aina yake.
Historia inatufundisha kwamba
hata wagunduzi walifanikiwa tu kwasababu waliweza kushinda hofu ya kufanya
jambo mara ya kwanza, na kwa kweli walifanikiwa baada ya maumivu makubwa.Thomas
Edison mvumbuzi wa taa za umeme[ki biashara] alifanikiwa kutengeneza balbu
baada ya kufanya majaribio zaidi ya elfu kumi.
yawezekana mtu akaja na hoja
kwamba, vipi kama sitaki kujaribu chochote,ukweli ni kwamba hili
haliepukiki,labda unaweza kufanikiwa kwa muda mfupi, lakini ukweli ulio
dhahiri ni kwamba mara ya kwanza ulizaliwa [ bila wewe kupenda] basi
unayo nafasi ya kujaribu mambo mengi,kwa mara ya kwanza na mara nyingine na
nyingine kwa kupenda,
kabla hujaondolewa[cleared] kwa
mara ya kwanza kutoka ulimwengu huu[vilevile bila wewe kupenda].Yaani kabla
hujafa,na kwa taarifa tu wengi wanaoishi sasa walishakufa [kwa
kupenda] wakiwa na miaka mitano, kumi, thelathini au arobaini;wanasubiri
kuzikwa[bila wao kupenda] wakifikia umri wa miaka sitini , sabini au
tisini.
0 comments: