Jihadhari na marafiki, kwani wanaweza kukusaliti haraka zaidi maana ni rahisi sana wao kukuonea wivu. Watu hao wanaweza kubadilika na kuwa wakatili. Ukianzisha uhusiano na mtu ambaye aliwahi kuwa adui yako utagundua kwamba atakuwa mwaminifu zaidi kuliko rafiki.
kwa vile atataka kukuthibitishia kwamba uhusiano wenu ni wa dhati. Kwa kifupi, waogope zaidi marafiki zako kuliko maadui.
Katika safari ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio na heshima, kuwa na maadui ni jambo muhimu kwani husaidia kuongeza ari na huthibitisha uwezo wako hasa pale inapotokea maadui hao wamesalimu amri kwako.
0 comments: