WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725
BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725
Jipime umefanya nini
kujenga mafanikio. Baada ya mihangaiko ya hapa na pale, kule na huko wakati
mwingine kushindwa hata kulala au kuhatarisha maisha yako katika safari
mbalimbali, jiulize je, umefanikiwa kupata kile ulichotaka?
kubishana
sio ukorofi inategemea mnabishanaje na kuhusu nini? Katika hali halisi
kubishana kwenye uhusiano kunahashiria afya ya uhusiano wenu....ikiwa kuna watu
wanaishi pamoja kama wapenzi na hawajawahi kubishana basi ni either
wanadanganya au mmoja wao anamuogopa mwenzie.
Jitengenezee
soko lako maalum. Kama ungependa biashara yako ifahamike kati ya biashara
nyingine ni muhimu kuwa na soko lako maalum linaloeleweka. Hii ni njia ya pekee
ya kukutofautisha na washindani wako.
Jijengee
mazingira ya kupata faida endelevu. Ikiwa unafanya aidha biashara ya huduma au
bidhaa, ni muhimu kutathmini bei ya bidhaa uliyopanga ili kupata faida
endelevu. Jiulize je bei uliyopanga inaendana na uhalisia katika soko?
Katika maisha, hakuna kinachoshindikina kama kweli
utaamua kwa dhati kukipata. Kinachochangia watu wengi kutotimiza kile
wanachokitaka maishani, ni kutodhamiria kwa nia na nguvu zote kufuatilia
malengo yao.
Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. uvivu wa kufikiri na wa kufanya
kazi unakwamisha maendeleo. tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi
kwa bidii.