Waafrika ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya maisha. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi na wadogo zake na kuwasomesha.
Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo hili
likawekwa sawa mapema. Je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa upande upi na
kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada ya kuoana?
Pale tu mtakapooana au lini? Hili si
jambo dogo na linaweza kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba. Ni vyema
mkaliweka sawa mapema na wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada
bali Mr & Mrs hivyo heshima iwe kwa wote.
Pia sishauri kuishi nao mara tu baadavya
kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza muweze
kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea nyumba yenu
mkiwa wenyewe.
0 comments: