Kwanza, jaribu kulipa zaidi ya kiasi unachodaiwa kila mwezi
kwenye kadi ya mkopo au deni lingine.
Pili, jitahidi kulipa deni linalodai ulipe riba ya kiasi
cha juu zaidi.
Tatu, dhibiti jinsi unavyotumia pesa. Hilo ni jambo muhimu sana.
Jifunze kuishi kulingana na mapato yako.
Deni la Lazima
Ni watu wachache wanaoweza kulipa
pesa taslimu kwa ajili ya nyumba wanayonunua. Kwa hiyo, wengi huchukua mkopo
kwenye benki ili kununua nyumba. Kiasi wanacholipa kila mwezi ili kurudisha
pesa hizo huonwa ni kana kwamba wanalipa kodi ya nyumba. Lakini baada ya kulipa
mkopo huo kwa muda mrefu, wanamiliki nyumba hiyo!
Pia watu wengi huona kuwa inafaa
kuchukua mkopo ili kununua gari ambalo halitumii petroli nyingi. Wanapolipa
mkopo huo upesi iwezekanavyo, gari hilo huwa na faida, na hiyo ni njia nyingine
ya kuokoa pesa.
Wengine wameona ni jambo la hekima kununua
gari la mtumba lililo katika hali nzuri na ambalo halijatumiwa sana. Wengine
huokoa pesa kwa kutumia usafiri wa umma au hata kuendesha baiskeli.
Vyovyote vile, uwe na kiasi na uone
mambo kihalisi kuhusiana na vitu unavyonunua na ufanye maamuzi ukiwa makini.
Unaweza kukuza tabia ya kutumia pesa bila hekima na hilo litakuletea matatizo.
Kwa hiyo, jitahidi kutumia pesa kwa uangalifu na kwa busara, na huenda ukafaulu
kuwa na furaha ya kudumu.
Mbali na hilo, ili ufurahie
kuhifadhi pesa, unapaswa kujua jinsi ya kuzitumia kwa hekima. Habari inayofuata
itazungumzia jambo hilo.
0 comments: