Hatua
muhimu za kuzingatia
1. Nyambulisha na
uainishe mradi unaotaka kufanya kwa msingi wa wazo
linalotekelezeka
2. Fursa ya
biashara hutokana na yafuatayo;
a. Tathmini ya wazo
lako la biashara.
b. Tathmini ya kina
ya mahitaji ya soko ambalo biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina
ya bidhaa zako na huduma zako.
d. Tathmini ya kina
na jinsi bidhaa yako/huduma yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na
ufafanue walengwa/watumiaji wa bidhaa au huduma zako.
f. Tathimini
taratibu za kisheria na kiutawala kuhusu biashara unayotaka kuanzisha.
3.
Angalia ushindani uliopo sokoni (husisha yafuatayo)
a. Angalia na
uorodheshe biashara nyingine zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka kutoa wewe.
b. Angalia na
ujiulize kama wapo washindani wengine wapya wanaotaka kuingia kwenye biashara
hiyo hiyo unayokusudia.
c. Jiulize
changamoto zilizopo na vikwazo vilivyopo (kisheria, kimtaji, au vinginevyo)
vinavyoweza kuzuia biashara nyingine zinazofanana na biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe
upekee wa bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za kumfanya mtu ahitaji
bidhaa/huduma yako badala ya bidhaa/huduma nyingine zilizopo sokoni)
asante sana kwa mafunzo haya ya mawazo ya biashara
ReplyDelete