Katika maisha, hakuna kinachoshindikina kama kweli
utaamua kwa dhati kukipata. Kinachochangia watu wengi kutotimiza kile
wanachokitaka maishani, ni kutodhamiria kwa nia na nguvu zote kufuatilia
malengo yao.
Lakini pia
woga huchangia kwa kiasi kikubwa sana. Kabiliana na hofu. Tunapokuwa waoga,
huwa tuna sizi kiakili, kimwili na kihisia na hushindwa kabisa kuchukua hatua.
Ni lazima uwe na sababu za kwa nini unataka kutimiza
lengo hilo maishani mwako. Ukiwa na lengo lisilo kuwa na sababu mara nyingi
huwa ni vigumu kulitimiza maana hakuna kitu kinachokusukuma katika kufanya
hivyo.
Hakikisha
unajikumbusha kila mara akilini mwako kuwa ni kwanini unataka kutimiza hilo
lengo maishani mwako. Sababu yako yakinifu ndani ya moyo ni chanzo cha hamasa.
Safi kabisa nimeelewa maana hata mm ni mmoja wapo
ReplyDeleteHakika ndugu ni sahihi
ReplyDeletepamoja
ReplyDelete