Images
JIFUNZE NAMNA YAKUPUNGUZA MAFUTA NAKUWEKA USO SAFI…!!!! SOMA HAPA
Ukiwa mwanaume au
mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili kukuweka mtanashati na
mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia kuondoa mafuta ambayo yana
kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub. Husaidia kuondoa chunusi, vipele
na makovu na pia inapunguza mafuta usoni. Uso
unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na
vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.Unaweza kutumia scrub kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku
tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa
kulingana na ngozi yako. safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha
chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha
nawa uso na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke. Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji
safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi. Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa
kutoa taka. Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya moto. Baada
ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano nyingine kisha nawa. Paka
poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya
kuufanyia facial uso wako Pia unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa
unanawa uso asubuhi na jioni hii huondoa upele, chunusi na mabaka usoni.
0 comments: