Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye
mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo
kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile
vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja.
Ni kweli kuna vingine huwezi
kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila
kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na
unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko
aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa.
Kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka
wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto
2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza
kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.....
0 comments: