Linganisha mapato na matumizi. Kama
mapato yote yanazidi matumizi basi bajeti hiyo uliyoiweka inakufaa bali kama
matumizi yamezidi mapato kaa chini uangalie lipi sio la muhimu uondoe au
upunguze fedha ulizozipanga. Ili uweze kuwa na bajeti yenye manufaa jaribu
kuweka mgawanyo wa fedha kufuatana na umuhimu wa jambo husika. Kwa mfano:
Fungu la kumi 10% (kuna wanaotoa
zaidi!)
Kodi ya nyumba 20%
Matumizi ya nyumbani 30%
Gharama za ofisini 15%
Binafsi 4%
Mavazi 3%
Burudani 3%
Matibabu 5%
Tahadhari 5%
Bajeti ya mavazi sio lazima itumike
kila mwezi bali unaweza kuweka na kuitumia kila baada ya muda fulani. Fedha za
matibabu tenga kila mwezi iwapo hazitatumika usitumie kwa shughuli nyingine
bali endelea kuziweka. Akiba ni kwa ajili ya mipango ya baadaye na dharura
kubwa, na ya tahadhari ni kwa ajili ya dharura ndogo yoyote.
0 comments: