Angalia uwezekano wa biashara yako kuendelea
na kukua (jibu yafuatayo)
a. Utawafikiaje
walengwa wa biashara yako (Ni kwa vipi walengwa wako watajua kuhusu bidhaa na
huduma zako)?
b. Utasambazaje/
fikishaje bidhaa/huduma zako (Bidhaa zako zitafikaje kwa wauzaji wa rejareja au
huduma zako zitafikaje kwenye maeneo uliyokusudia na maeneo hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio
yako ya wafanyakazi unaohitaji kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi wangapi utahitaji
mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye
nini ili biashara yako ipate faida na itachukua muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio
yako ya mapato na matumizi kwa miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi gani
katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, wa tatu na wa nne)?
f. Unahitaji mtaji
wa kiasi gani (kiasi gani cha fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa kwanza,wa
pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha biashara yako?
g. Utawezaje kupata
kiasi hicho cha mtaji? Je ni kwa kuanza kuweka akiba katika benki au kuomba
mkopo na kwa gharama gani?. Je mchango wako katika mtaji ni kiasi gani? Je
mradi wako unaweza ukabeba gharama zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha faida?...
0 comments: