Jifunze namna bora ya kuandika mpango mkakati kwa ajili ya kikundi, ofisi au shirika lako. Ili uweze kuandika Kuandika Mpango Mkakati, kwanza tujue mpango mkakati ni nini na unatakiwa wakati gani?
Mpango mkakati ni taarifa iliyoandikwa kwa lugha
rahisi kueleweka yenye kuonyesha dira ya taasisi husika na mambo gani yatawekwa
kipaumbele katika kipindi cha miaka 3 hadi mitano ijayo. Taarifa ya mpango
mkakati ni lazima pia ionyeshe rasilimali fedha, watu na vitu vitakavyotumika
kufikia maono au dira
Wakati
gani mpango mkakati unatakiwa
Ni pale tu taasisi inapotaka kufukia kwa ufanisi
lengo fulani au pale taasisi haifanyi vizuri kwenye matumizi ya muda, fedha,
watu na vitu na pia imebainika wazi kuwa malengo hayataweza kufikiwa.
Hii inaweza kufahamika tu kama taasisi itaamua
kujitadhmini. Ili kufaahamu zaidi ni wakati gani huu mpango unahitajika hebu turudi
nyuma kweny mwanzo wa kutumika neno mkakati wambao ndio msingi mkuu wa neno
Mpango mkakati.
Hili neno lilianza kutumika vitani, jeshi
lilipozidiwa na maadui walirudi nyuma na kujiwekea mkakati wa kurudi vitani na
kushinda vita
Hatua
za kuandika mpango mkakati
Hatua
ya kwanza
A:
Uchambuzi yakinifu wa mahitaji
Watumiaji wakuu wa mpango mkakati ni taasisi husika.
Kama mshauri na mtaalam unatakiwa kufanya uchambuzi wa mahitaji ya msingi.
Katika hili zoezi utagundua hasa wadau wako wanahitaji nini?
Namna
ya kufanya uchambuzi
1. Kutumia
madodoso ili kupata maoni ya wadau wa taasisi
2. Vikao
vya faragha na viongozi muhimu
3.Mkutano
na wadau wote
Hatua
ya Pili
B: Ukusanyaji wa taarifa/takwimu na kazi katika
vikundi
Kutengeneza Maono, Wito, Malengo mahsusi, Maadili ya
msingi, viashiria vya ufanisi, Tadhimini nk
Kazi hii itafanywa kupitia uwezehswaji na kazi za
vikundi
Hatua
ya Tatu
C:
Kuandika Rasimu ya Mpango Mkakati
Kazi hii ili iende haraka inatakiwa kuandikwa na
mtaalamu kwa kutumia taarifa zilizopatikana kutoka kwa wahusika wenyewe
0 comments: