Uchumi ni sekta ambayo huchochea kwa namna moja au nyingine
maendeleo ya mwanaadamu. Biashara ni moja ya sehemu kuu ya uchumi na
maiongiliano makuu ya uchumi hupatikana kwa kupitia biashara,miradi na kwa
ujumla Ujasiriamali. Kufanya ujasiriamali ni moja katika njia za kujipatia
kipato.
Kwa kuzingatia haya pamoja na uhitaji wa dhana hii kuna
changamoto juu ya ufahamu na ujuzi maalumu juu ya Biashara, miradi na ujasiriamali
katika ujumla wake. Ujasiriamali ni ujuzi kama zilivyo tasnia nyingine, lazima
usomwe na kufunzwa kila anayetaka ufanisi wake na matunda yake.
Dhana inayojengeka miongoni mwa jamii kuwa ujasiriamali ni
swala la kipaji cha kuzaliwa nacho, kurithi au kujulikana pasi na elimu ni
dhana potofu inayowakwamisha wale wanaotaka kuchukua hatua kuufanyia kazi
ujasiriamali.
Mjasirimali mmoja anasema maneno yafuatayo. Mengi katika
usikiayo kuhusu ujasiriamali sio sahihi. Si uchawi; si mazingaombwe; na hauna
lihusianalo na maumbile, ni nidhamu na, kama nidhamu nyingine, Inawezekana kwa
kusomwa.
Usiogope kujiingiza kwenye ujasiriamali kwani uwoga wako
ndio umasikini wako…..
0 comments: