Images
KUFANYA TATHMINI YA MAFANIKIO ULIYOPATA INASAIDIA KUJUA WAPI UMESHINDWA..!!! SOMA HAPA
Jipime umefanya nini
kujenga mafanikio. Baada ya mihangaiko ya hapa na pale, kule na huko wakati
mwingine kushindwa hata kulala au kuhatarisha maisha yako katika safari
mbalimbali, jiulize je, umefanikiwa kupata kile ulichotaka?
Lazima ifike mahali
ujifanyie tathmini ya kile amabacho umefanya kwa siku, juma mwezi au mwaka,
epuka kufanya mambo kimazoea kwa kuwa tu unapata hela ya kula na kukidhi
mahitaji yako mengine, ni muhimu kwa wajasiriamali kujipima wenyewe.
Tunapozungumzia kupima mafanikio katika biashara yafaa
kutofautisha na ile hali ya wewe kukidhi mahitaji yako ya msingi kama vile
chakula, mavazi, malazi na matibabu. Kaa chini uangalie nini umepata na kwa
kiasi gani na kama ilipasa ufike hapo au zaidi.
Lakini kwa mjasiriamali kupima mafanikio ni kuangalia
mtiririko mzima wa kile ulichofanya kwa kipindi fulani. Unapojifanyia tathmini
ya mafanikio yako pia ni moja ya njia ya kuweza kuangalia pale ambapo
ulishindwa, na kujua nini kifanyike.
safi sana, nimepata kitu kwenye post hii, barikiwa sana.
ReplyDeleteDah? Kweli kaka kufanya kitu kwa mazoea ata ukianguka ujui nni kilicho kuangusha asante sana post hii akika imebeba mambo mengi sana
ReplyDelete