Jambo
moja jema hufukia mabaya mengi yaliyofanywa na mtu. Wema na ukarimu unaofanywa
kwa moyo mkunjufu humvutia hata mtu aliyekuwa na wasiwasi na wewe.
Wema
huo uliopangwa unapowavutia watu, ni wazi unaweza kuwalaghai na kuwatumia jinsi
utakavyo. Zawadi yoyote inayotolewa kwa muda unaotakiwa inaweza kufanikisha
lengo lako la kumtumia umtakaye kwa faida yako.
Epuka
kukumbusha wema wako mbele ya jamii, acha kuutumia wakati wa kuomba msaada. Unapotafuta
msaada kutoka kwa rafiki, usitake kumkumbusha misaada au vitendo vyema
ulivyomfanyia.
Ukimwambia
hivyo anaweza akakupuuza, badala yake mweleze kitu kipya katika kuomba msaada
huo au katika uhusiano wenu, kitu ambacho kitamnufaisha. Kisisitize kitu hicho
kwake.
Atakusaidia
kwa furaha mara atakapoona kuna kitu ambacho naye kitamnufaisha. Jifanye rafiki
wa mpinzani wako, lakini fanya kazi naye kama jasusi.
Ni
muhimu kumfahamu vyema mpinzani wako, ufahamu huo utaupata pale utakapoamua
kuwa rafiki wa adui yao na kutumia ukaribu huo kuchunguza mbinu zake ili
baadaye umshinde kwa udhaifu wake utakaoujua.
0 comments: