Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Je..!!! Nataka Kuacha Shule kwanza Unahitaji kufikiria mambo yafuatayo..... Soma hapa...

MWI-Lilongwe-1203-037-v1 (anthonyasael) Tags: africa unicef school girls boy portrait people black cute boys girl smile smiling horizontal kids writing notebook children happy reading chalk kid student uniform child emotion classroom affection desk african board happiness southern portraiture malawi program friendly learning anthony afrika teaching schoolchildren lesson studying blackboard primary pupil schoolage pupils schoolboy schoolchild cfs lilongwe emotionally topb asael


Ni kiwango gani cha chini zaidi cha elimu kilichowekwa na sheria katika eneo lenu? Umefikia kiwango hicho? Ukipuuza shauri la ‘kujitiisha kwa mamlaka zilizo kubwa’ na kukatiza masomo yako kabla ya kufikia kiwango kilichowekwa na sheria, basi unaacha shule.



Umetimiza malengo yako kuhusiana na elimu? Ungependa elimu ikusaidie kutimiza nini? Hujui? Unahitaji kujua! Ikiwa hujui, utakuwa kama mtu anayesafiri katika gari-moshi lakini hajui anakoenda. Ukikatiza masomo yako kabla ya kutimiza malengo yako kuhusiana na elimu, na ambayo wewe na wazazi wako mmeweka, basi unaacha shule.

Kwa nini unataka kuacha shule? Huenda baadhi ya sababu zikawa kuitegemeza familia yenu kiuchumi au kufanya utumishi wa kujitolea. Sababu za kibinafsi zinaweza kuwa ni kuepuka mitihani au kazi za shule. 

Tatizo ni kutambua sababu hasa inayokuchochea, na ikiwa ni sababu nzuri au ina ubinafsi. Ikiwa unaacha shule kwa sababu tu unataka kuepuka matatizo, utashangaa. Kuacha shule ni kama kuruka kutoka kwenye gari-moshi kabla ya kufika unakoenda

Huenda safari yenyewe ikawa yenye kuchosha na huenda hata wasafiri wasiwe wenye urafiki. Lakini ukiruka na kutoka, hutafika unakoenda, na huenda ukaumia. Vivyo hivyo, ukiacha shule, haitakuwa rahisi kwako kupata kazi.

 Na hata ikiwa utapata, huenda ukapata mshahara au malipo ya chini kuliko yale ambayo ungepata kama ungemaliza masomo yako.

Badala ya kuacha shule, jifunze kushughulikia kwa subira matatizo unayokabili shuleni. Ukifanya hivyo, mwishowe utagundua kwamba matokeo yatakuwa mazuri kwako.


0 comments: