Kama umefanikiwa au
unaelekea kwenye njia ya mafanikio sasa au ndio kwanza unaanza biashara
unatakiwa uwe na malengo, hapa nimejaribu kuweka chini dondoo za jinsi ya
kutawala mafanikio yako kibusara zaidi:
1. Sherekea mafanikio yako.Yawe madogo au
makubwa haijalishi mafanikio yanatakiwa ya sherehekewe. Haijalishi umetangaza
kwa umma au umealika marafiki wachache
na kuwashirikisha. Kusheherekea mafanikio ndio msingi
wa kufanya njia kwa mafanikio mengine makubwa zaidi. Dunia ina jinsi
inavyojiendesha na sisi tuna jinsi ya kuwasiliana na dunia kiasilia.
2. Usifiche hisia zako za kweli kuhusu hayo
mafanikio. Usijilahumu na kusema ulikuwa hustahili hayo mafanikio, badala yake
jieleze ulikuwa unastahili mafanikio hayo madogo au makubwa uliyaangaikia na
kufanyia kazi na hivyo sio bahati,
Wengi hupenda hujumu kuwa
mafanikio walipata na kusema ilikuwa bahati lakini wanasahau kuwa nguvu ya
akili iliyofichika(unconscious mind) na utendaji wake na kufanyia kazi maamuzi kwa akili iliyo
makini(conscious) ambayo ni asilimia 10% ya akili yote ya mwanadamu.
3. Weka dhamira ya kuhitaji zaidi ya hapo
usiridhike:Hatua ya mafanikio uliyofikia ndogo
ya mafanikio ,usione umefika mwisho na kushindwa weka juhudi
zaidi,Ngangania na fuatisha ndoto na malengo yako ya kukua kibashra na maisha
yako ambayo kila siku unayatafuta.Chukua muda wa kujifunza mambo mengine mapya
kuhusu kiwanda ambacho upo(sekta)au jifunze biashara mpya ambayo itakayo
fanikisha baadae yako.
4. Jifunze kutoka katika mafanikio yako.Kama
tunavyo ambiwa tujifunze kupitia makosa yetu,chukua muda kujifunza katika
mafanikio yako.Kipi sahihi ulifanya mpaka kikakufanya uwe hapo leo?Kiasi au
sehemu gani ya hayo mafanikio yamekufanya uwe na furaha sana?
5. Amua kama unataka baki katika hatua
uliyopo au kukua zaidi biashara yako.Punde baada ya kupata mafanikio makubwa ni
muda wa kuamua kuwa umefikia hatua uliyokuwa unaiota kila siku au una malengo
mengine ambayo bado unahitaji kufanikisha.
Mara kadhaa mafanikio ni kama kupanda
ngazi,kuna hatua baada ya hatua,wakati ukimaliza hatua moja unapanda nyingine
kusonga mbele,mathalani unafika hatua na kugundua uliyatengeneza maisha ya sasa
miaka mitano iliyopita na kipindi chote hicho ulikuwa makini sana na kutimiza
hayo malengo na ili uwe na uhakika wa kesho inabidi tuweke malengo sasa.
6. Tengeneza ulingano wa akiba kati ya
maisha yako binafsi na maisha biashara yako.Mafanikio huja baada ya kujitoa
muhanga mtu binafsi katika biashara husika.Chukua muda wako sasa na angalia
wapi katika kipindi cha uhai na kuweka ulingano katika maisha yako na
biashara,isije siku ikawa unamafanikio sana upande mmoja mwingine hauna
.Tengeneza maisha yenye mafanikio sio tu biashara yenye mafanikio.
7. Chagua fursa sahihi/za uhakika zinazokuja mezani kwako, epuka
mawazo mazuri ambayo hayata saidia biashara yako kushamiri au kukua kwa
biashara yako.
Katika hatua kubwa ya
mafanikio, kupaniki ni tabia ambayo siyo
ya kuipatia nafasi hata punde, kuondoka kwa hofu kunakupatia wewe kuamua kama
fursa iliyokuja ni ya kweli(uhakika kwa wewe) ambayo itasogeza mbele biashara
kimafanikio au ni wazo tu nzuri ambalo halitakusaidia kukua au kufanyika kwa
muda huo/na wewe.
8. Shirikisha stori ya mafanikio yako kama
somo wengine.Chukua muda wako kuwafundisha somo la mafanikio yako wenzako au
wengine,ili waweze kujifunza kutoka mafanikio na mambo uliyopata
shindwa.Rudisha fadhila kwa jamii na watu ambayo ndio kwanza wanaanza kama njia
ya kushirikisha au kushiriki kwa pamoja busara na imani yako juu ya mfanikio
9. Tizama jinsi ofisi yako inavyofanya
kazi.Je kuna mabadiliko yanahitajika?je kuna lolote linaweza kuendeshwa moja
kwa moja?sasa ni muda wa kuweka nguvu zako zote katika utawala/uongozi wa
kampuni yako,ili iweze jiendesha vema baadae.
10. Tengeneza mradi biashara(business plan) na
malengo ya miaka mitano.Nini kitafuata kwako na biashara yako?ni muda wa kukua
zaidi na zaidi?kuchanja mbuga mwelekeo tofauti?kutoa bidhaa na huduma tofauti
ili kutengeneza vyanzo tofauti vya biashara yako?kusimamisha kuuza bidhaa na
huduma chini ya kiwango?
11. Weka jicho kwa waharibu maono/maadui/wenye
chuki.Kuna watu katika maisha yako huchukia wewe ukifanikiwa kwa sababu ya wivu
au vitisho.Weka umakini juu ya watu wanvyoonyesha hisia zao juu ya mafanikio
yako.Mara zote jichangane na watu ambao kweli wanafurahia mafanikio yako na
mambo ambayo unfanya .Epuka kuka na watu wenye chuki na wewe.
0 comments: