Migogoro mingi baina ya walio kwenye uhusiano husababishwa na wenzi kutowafahamu vyema wenzao. Usiingie katika mkumbo huu, ni suala la kujieleza tu. Kumweleza mpenzi wako ulivyo, kutamfanya ajue vitu unavyopenda na usivyopenda. Aidha, kama unao udhaifu wowote wa kiafya na kadhalika, mweleze mwenzako.
Kumweleza kutamfanya ajiamini kuwa
anapendwa. Kunaonesha unavyojiamini na unayetaka mwenzako ashirikiane na wewe
katika hali uliyonayo. Si vibaya mwenzio kukufahamu kwamba una hasira sana.
Yes! Maana akishajua hilo, ataacha utani unaokaribia kukuudhi maana anajua
vizuri kuwa una hasira za karibu.
Ipo mifano mingi sana, lakini kikubwa cha kushika katika kipengele hiki ni kuwa mkweli kwa mwenzako kuhusu maisha yako. Acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa, wakati ni wa kawaida.
Kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni
hazina iliyojificha ndani ya moyo. Kama anakupenda, anakupenda tu! Siku
akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka
ndani ya moyo wako. Naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa
kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro.
0 comments: