Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini,
Ni Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako. Jifunze Kusoma Hisia Za
Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya
Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake.
Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo
Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata Mnapokuwa
Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia
Penzi Lako Na Manjonjo Yote Unayomfanyia.
Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza
Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa
Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya.
Kwa Maneno Mengi wewe Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya
Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na Nini Hapendi Ili Uweze Kuwa mwanaume
Bora, Maana Hata Hisia Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu.
Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila
Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo Hana
Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua Kitu
Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia Utaona.
Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote,
Lakini Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha
Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna
Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine.
Hapo Sasa Unaweza Kuibuka mshindi Maana Utakuwa
Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi
Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza Kuzifanyia Kazi.
0 comments: