Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

USITEGEMEE BAHATI KWENYE BIASHARA YAKO..!!! SOMA HAPA





Kufaulu ama kushindwa kwa biashara kuna tegemea mambo mengi. Kwanza huenda ikawa tatizo la aina ya biashara yenyewe nikiwa na maana kwamba ni biashara ambayo si endelevu. 


Ndiyo maana utafiti juu ya uhitaji wa huduma ama bidhaa ni muhimu sana. Kwa biashara ambayo ni kubwa na muhimu kwa wote suala linakuja pale ambapo kuna wachache wanaoamua karate zichezwe vipi. Hapa ninalenga kwa biashara za kitaifa na kimataifa.

Shida kubwa tuliyonayo wengi ni suala la kuiga mawazo ya kibiashara kwa hiyo kukosekana kwa ubunifu kuna sababisha biashara nyingi kutofanikiwa. Kwamba kunakuwa na utitiri wa watu wanaofanya biashara moja na hivyo kutoiletea mvuto biashara husika.

Elimu ya biashara kwa wengi tatizo. Biashara pia ni sanaa, yaani hapa tutambue kwamba inahitaji ujanja wa namna ya kuimudu na kuiwekea nguvu na mvuto wa aina yake na hivyo kuwa na wateja wengi na uhakika, kwa hiyo si suala la kuvamia tu.

Kukosekana kwa uaminifu ni tatizo kubwa hasa kwetu weusi. Hatuaminiani na pia tuna ubabaishaji mwingi. Biashara inahitaji kujitoa, kuwa na subira na pia kuwa na uaminifu wa hali ya juu. Tunahitaji kuwekeza kila kinachohitajika kwa kile tunachoamini kuwa kitatuletea kipato halali.

Mazoea kwenye biashara na kukosekana kwa tathimini makini ni ugonjwa sugu.Tunachelewa kutambua kwamba tufanyavyo sivyo. Na kwamba tunaridhika mapema na kwa mafanikio kidogo.

Bahati ipo lakini nafasi yake siyakuzingatiwa. Kwamba huwezi kufanya biashara kwa kutegemea bahati. Hapa niseme labda suala la risk na uncertainty sijui kwa Kiswahili niliiteje, ile hali ya kutojua yatayojiri baada ya kuchukua hatua ya kuianza biashara husika.

Lakini kwa kufanya utafiti wa kina kabla na pia kuwa bima ya biashara ni muhimu ili kuwa salama pale yanayopokuwa yamekwenda kombo.

 


1 comment:

  1. Kaka unafundisha nini kuhusu suala la kuiga mawazo ya mtu mwingine? hiyo makala yangu ya nini nini hasa unachohitaji ili ufanikiwe kiuchumi hukuiiba kutoka tovuti ya KUELEKEAUTAJIRI?, mbona hukutumia kanuni ya kutoa japo credit kwa source wa makala yenyewe, tuache unafiki tujitahidi KUPRAKTISI yale tunayofundisha.

    ReplyDelete