Waweza kufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na
afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula
chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni
asali na mdalasini.
Unachohitajika
kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vile vile,
wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili
kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na
kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu.
Rudia mchanganyiko huu
kabla ya kulala. Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana
na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni
muafaka.
Pia kinywaji
hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya
kula pamoja na kuleta joto mwilini.
0 comments: