Mwanamke anafananishwa
na meli ya biashara kwa sababu meli ya biashara inachukua bidhaa mbali mbali
ndani yake, Mwanamke amebeba majukumu mengi sana katika maisha yake, mwanamke
huyu ni:-
a) Mlinzi wa Mume wake.
b) Mzazi, mlezi mwenye
watoto.
c) Mwangalizi mkuu wa
familia yake na mazingira yake
d) Mwalimu Mkuu wa
familia yake
e) Adui wa maadui wa
familia yake.
f) Muombaji wa familia
yake.
g) Kisima cha amani
katika familia na ndugu wanaomzunguka.
h) Chanzo cha Baraka ya
familia
i) Mficha siri ya
familia- najua unajua kuwa Mwanamke ndio mficha siri wa familia anajua yote
yanayofanyika ndani. Mwanamke ana majukumu mengi sana huku mtoto analia,
baba naye anamwita huku
watoto wanataka kusoma, wakwe wanataka chakula na mavazi huyu anatakiwa
kusaidiwa lakini Mwanamke wa namna hii ndiye anayetakiwa katika maisha yako
ndiyo maana amefananishwa na meli ya biashara malalamiko amepewa yeye matusi
yeye, sifa njema yeye Mwanamke ni gari la familia. Nyumba yenye heshima
inamuhitaji Mwanamke sahihi.
0 comments: